Miss Tanzania Ajitapa Kutwaa Taji la Miss World

Miss Tanzania akijitapa kurudi na taji la Miss World kwenye kinyang’anyiro hicho.

Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tanzania 2019-2020 Silyvia Sebastian amejitapa mbele ya Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, kurudi nchini na taji la Miss World kwenye kinyang’anyiro kinachofanyika katika jiji la London chini Uingereza hivi wiki ijayo.

Waziri Mwakyembe akizungumza kabla ya kumkabidhi Miss Tanzania bendera ya taifa.

Silyvia alisema hayo jana wakati jioni akikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri Mwakyembe katika Mgahawa wa The Grand uliopo Posta, Dar kwa ajili ya kwenda kuliwakilisha taifa.

Waziri Mwakyembe akimkabidhi bendera Miss Tanzania, Silyvia Sebastian.

Akizungumza na wanahabari amesema kwa kushirikiana na kampuni ya The Look waandaaji wa michuano hiyo wamejiandaa vya kutosha kufanya maajabu kwenye michuano ya mwaka huu yanayoshirikisha warembo 130 kutoka mataifa mbalimbali.

Mkurugenzi wa The Look, Basilla Mwanukuzi akiwaomba wadau kumpigia kura Miss Tanzania atakapokuwa kwenye michuano hiyo.

Waziri Mwakyembe, Miss Tanzania na wadau wengine waliofika kwenye mgahawa huo kushuhudia makabidhiano hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

HABARI: NEEMA ADRIAN
PICHA: RICHARD BUKOS

RAIS MAGUFULI ALIVYOSHIRIKI MISA YA JUMAPILI LEO


Loading...

Toa comment