Miss Tanzania Akwaa Skendo UDM

Mary Peter.

MISS Tanzania namba mbili 2016/17 ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar (UDSM), Mary Peter amekwaa skendo ya kimapenzi baada ya kudaiwa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwenzake ambaye pia ni Mr Tanzania 2017, Davies Machumilane.

 

THE PUNCH lilipenyezewa ubuyu kuwa, Mary ambaye pia ni Miss Mwanza anayechukua masomo ya Sociology chuoni hapo, amekuwa akionekana mara kwa mara ‘very close’ na Davies na hata wakati mwingine huonekana nyakati za usiku maeneo hayo ya chuo wakiwa katika mapozi ya kimahaba.

“Mwanzoni walikuwa wakifanya kwa siri lakini sasa ipo wazi kabisa, ni wapenzi naona wameamua kuchukuana kutokana na wote ni washindi wa mashindano ya Mr na Miss,” kilisema chanzo.

Davies Machumilane.

 

The Punch lilimtimbia Miss huyo hadi chuoni kwake kupata uhakika wa madai hayo ambapo alipopatikana mrembo huyo alifunguka;

“Kuwa katika uhusiano ni kitu cha kawaida mbona! Nipo katika uhusiano lakini si na Davies,” alisema Mary.

 

Alipotafutwa Davies kujibu hili, alifunguka;

“Alivyokwambia ni hivyohivyo, Mary ni mtu wangu wa karibu sana, tumezoeana sana labda ukaribu huo unafanya watu waone ni wapenzi.”

Na Andrew Carlos | The Punch.


Toa comment