MISS TZ ANA BIFU NA BASILA?

Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth

BAADA ya stori kusambaa kuwa Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth ameingia kwenye bifu na mratibu wa shindano hilo, Basila Mwanukuzi na kwamba hajapatiwa hata pesa ya kwenda kushiriki Miss World, mwenyewe amefunguka kuwa wapo sawa.  

 

Katika stori hizo zilizosambaa, ilidaiwa kuwa baada ya kufanyika Miss Tanzania 2018, kuna kiasi cha pesa alichokuwa akitakiwa kupewa mshindi huyo na Basila kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea Miss World, lakini hakupewa.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Queen Elizabeth alisema, hana ugomvi wowote na Basila na maneno yanayoongelewa na watu yana lengo la kutaka kuwagombanisha.

 

“Ningeomba niweke wazi kuwa sina matatizo yoyote na mratibu wa shindano langu, Basila Mwanukuzi, tena ninampenda sana, nipo naye vizuri tu, ningependa maneno yanayoongelewa na watu yapuuzwe, tuangalie mambo ya maendeleo ili tuweze kufika mbali zaidi na kuitangaza nchi yetu,” alisema Queen.

Stori: Zaina Malogo

Loading...

Toa comment