The House of Favourite Newspapers

MISS TZ: SICHAGUI, NITAFANYA CHOCHOTE CHA KIJAMII

Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth

BAADA ya kurudi kwenye mashindano ya Miss World ambako hakufanya vizuri, Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth amesema kuwa, yuko tayari kufanya chochote kati ya filamu, muziki na ujasiriamali. Mrembo huyo aliliambia Za Motomoto News kuwa, anajigamba kuwa atafanya chochote kwa kuwa ana uwezo katika kazi zote alizotaja.

Alisema kuwa, hawezi kujifunga kwenye kitu kimoja na siku zote ana imani kwamba wanaofanikiwa wengi wanafanya vitu zaidi ya kimoja. “Mbali na kuwa Miss Tanzania kwa mwaka huu 2018, niseme tu kwamba mimi ni muigizaji mzuri na ninao uwezo pia wa kuimba. Kwa hiyo siwezi kusema nitafanya muziki au filamu, chochote kitakachokuja mbele yangu nitaanza nacho, hata ujasiriamali pia uko kwenye damu,” alisema Queen.

Kuhusu kushindwa kufurukuta kwenye mashindano ya Miss World yaliyofanyika hivi karibuni Sanya nchini China, mrembo huyo hakuwa tayari kuongea lolote akidai haukuwa muda muafaka.

Stori: Memorise Richard

Comments are closed.