Miss Tanzania 2018: Ushindi wangu Ulibaki Kwa Watanzania

Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune (kulia).

Baada ya mashindano ya Miss World kukamilika na Queen Elizabeth Makune ambaye ameiwakilisha Tanzani kwa mwaka 2018, amesema kuwa kazi yake aliifanya vyema na kwamba kazi pekee ilibaki kwa Watanzania kupiga kura.
Makune amefunguka hayo wakati wakati wa hafla ya kujipongeza pamoja na familia yake baada ya kutoka kwenye mashindano ya hayo ya walimbwende duniani, ambapo amesema kuwa kukosa taji hilo haimaanishi hakuwa na sifa.

“Kazi yangu niliikamilisha vyema na na mengine yalibaki kwa nchi yangu kupiga kura na vitu vingine kama hivyo, na nilikamilisha kila kitu kwa kadri ya uwezo wangu”, amesema Queen Elizabeth.

Mashindano ya Miss World yalifanyika Disemba 8, mjini Sanya nchini China, ambapo taji hilo alilitwaa mrembo kutoka nchini Mexico Vanessa Ponce, na kutoka Afrika lilitwaliwa na mrembo kutoka nchini Uganda Quiin Abenakyo.


Loading...

Toa comment