The House of Favourite Newspapers

Elice Mwakanjila Aibuka Kidedea Miss Ustawi 2017

0
Miss Ustawi wa Jamii, 2017, Elice Mwakanjila baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Ukumbi wa King Solomon, Msasani, Dar usiku wa kuamkia leo.
Elice Mwakanjila (katikati)  akiwa na mshindi wa pili, Ruth Deogratius (kushoto) na mshindi wa tatu, Melody Thomas (kulia).
Meya wa Manispaa ya  Kinondoni na Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Miss Ustawi.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akiongea neno baada ya washindi kupatikana.
Miss Ustawi wa Jamii, 2017, Elice Mwakanjila akisalimia.

 

Benjamin Sitta (kulia) akimkabidhi cheti mwandishi Musa Mateja wa Gazeti Pendwa la Amani, linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd  kutokana na kudhamini shindano hilo.
Mtangazaji wa Global TV Online, Isri Mohammed (kulia) akifanya mahojiano na Elice Mwakanjila.
…Akifanya mahojiano na mama mzazi wa mshindi.
Warembo waliotinga Tano Bora.
Warembo wote walioshiriki Miss Ustawi wa Jamii 2017.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’ akifanya yake.
Mgeni rasmi Meya wa Kinondoni,  Benjamin Sitta (katikati) akifuatilia warembo wakipita jukwaani (hawapo pichani).
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja.

MWANAFUNZI wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Elice Mwakanjila usiku wa kuamkia leo Jumamosi, ameibuka kinara wa Miss Ustawi 2017, baada ya kufanya vyema na kuwapiku wenzake 10 aliokuwa akishindana nao kugombania taji hilo.

Ishu nzima ya tukio hilo ‘ilihapeni’ katika Ukumbi wa King Solomon, Namanga jijini Dar ambapo Elice alichaguliwa kuwa mshindi baada ya kufanya vyema kwenye vipengele vya kusakata rhumba, kutoka na vazi la ufukweni na kumaliza shoo na vazi la jioni.

Elice alichaguliwa kuwa kinara wa wenzake na orodha ya majaji wakiongozwa na Jaji Mkuu, Happiness Watimanywa. Ruth Deogratius akibeba nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Melody Thomas.

Katika shindano hilo mgeni rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta, ambaye aligawa vyeti kwa baadhi ya wadhamini waliokuwa wakiliwezesha shindano hilo na miongoni mwa wadhamini hao ni Gazeti Pendwa la Amani linalochapishwa Kampuni ya Global Publishers ltd na kuwa mitaani kila Alhamisi. Cheti hicho kilipokelewa na mwandishi wa gazeti hilo, Musa Mateja.

(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

Leave A Reply