MISS UTALII WALAMBA SHAVU NONO

Ofisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Geoffrey Nago (kushoto) akielezea umuhimu wa shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania 2019/2020 ambalo limepata baraka zote kutoka katika taasisi yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Jaromax Palace Hotel ya Dar es Salaam, Thomas Fusi.

SHINDANO la Miss Utalii limeingia makubaliano ya kudhamini shindano la Kimataifa la Miss Utalii Tanzania 2019/2020 na hotel ya kitalii ya Jaromax Palace Hotel ya Dar es Salaam. 

Mkurugenzi wa mashindano hayo, Georgina Saulo,  amesema wameingia makubaliano hayo ili kufanikisha sera ya taifa ya utalii na uungaji mkono kwa vitendo wa jitihada kubwa zinazofanywa na serikali.

Mkurugenzi wa mashindano hayo na matukio, Georgina Saulo.

“Tumeamua kuungana na hoteli hii kwa sababu ni uthibitisho wa hadhi na ubora wa hoteli hiyo na huduma zake ambazo ni za kitalii na pia shindano letu litakuwa linahusha vitu vya Kiafrika yakiwemo mavazi yatakayovaliwa na tamaduni zetu za  Afrika, hivyo kulifanya shindano hilo kuwa la kimataifa likishirikisha washiriki wa ndani na nje ya nchi, na kupanua wigo wa wawekezaji, wafanyabiashara na nchi kujitangaza kimataifa kupitia shindano la washiriki kutoka nchi mbalimbali,” alisema Georgina.

Matukio katika picha:

Balozi wa Hoteli ya Jaromax Palace, Bathoromeo Julius,  akizungumza na wanahabari.

Kamati ya Miss Utalii na uongozi wa hoteli ya Jaromax Palace.

Sehemu ya vyumba vya hoteli hiyo ya kisasa.

Mandhari ya nje ya hoteli hiyo.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN


Loading...

Toa comment