MISS UTALII WASAKA WARATIBU KANDA

BAADA ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kupitisha mfumo mpya wa uongozi na kuruhusu tena shindano la Miss Utalii, limerejea tena kwa mara nyingine nchini ambapo kwa sasa linasaka waratibu wa kila kanda.

 

Akizungumza na mtandao huu, Mwenyekiti Mtendaji wa Mashindano ya Miss Utaliii, Erasto Gideon alisema kuwa, hadi sasa wanatafuta waratibu katika kanda nane.

 

“Kanda hizo ni Kanda ya Kaskazini (Manyara, Arusha na Kilimanjaro), Kanda ya Kusini (Ruvuma, Lindi, Mtwara na Morogoro), Kanda ya Pwani (Dar na Tanga), Kanda ya Magharibi (Kigoma, Tabora na Katavi), Kanda ya Ziwa (Mwanza, Kagera, Mara, Geita na Simiyu).

“Kanda nyingine ni ya Kati (Dodoma, Singida na Shinyanga), Kanda ya Nyanja za Juu Kusini (Mbeya, Rukwa, Iringa na Njombe) pamoja na Kanda ya Mashariki (Unguja na Pemba),” alisema Gideon.

Sifa kuu za waombaji ni pamoja na kusajiliwa na Basata pamoja na BRELA. Kuwa na kiwango cha elimu kisichopungua digrii, kuwa na ofisi ya kudumu katika moja ya mikoa ya kanda husika, kutokua na rekodi za uharifu na ukiukwaji wa maadili.

Kwa maelezo zaidi wanaweza kuwasiliana kwa namba; 0754882805/0658373337. Mwisho wa kupokea maombi ni Julai 17, mwaka huu.

Imeandaliwa na Stella Kasabo

MAJERUHI WA AZAM HOI KITANDANI AZUNGUMZA – VIDEO

Loading...

Toa comment