MISS WA BONGO ALIYENASWA KWA SANGOMA NAKAAYA AANIKA
DAR ES SALAAM: Kwa wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii, video ya mrembo aitwaye Samirata anayetajwa kuwahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania miaka ya nyuma, akiwa kwa mganga ndiyo gumzo huko mtandaoni, Risasi Jumamosi limefanikiwa kuzungumza msanii wa Bongo Fleva, Nakaaya Sumari ambaye ameanika ukweli wa jinsi alivyohusishwa na kusambaa kwa video hiyo.
Video hiyo inayomuonesha mrembo huyo akiwa kwa sangoma ilizua mshangao wa aina yake mapema wiki hii katika mitandao ya kijamii, huku lawama zikiporomoshwa kwa Nakaaya akidaiwa kuwa chanzo cha kusambaa kwake.
TUICHAMBUE KIDOGO VIDEO
Video hiyo ilimuonesha mrembo huyo akiwa amekaa kwenye kiti kilichoundwa kwa miti, chini ya mti mkubwa akiwa amevaa kanga moja, mkononi akiwa ameshika kuku, miguu ikiwa imekanyaga nazi, pembeni kukiwa na mayai na tunguli huku mganga akiwa bize kumpaka dawa katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.
MANDHARI
Mandhari ya video hiyo yanaonesha ni ya porini na wakati mganga huyo akiwa bize kumpaka dawa, pembeni yao alionekana amekaa mwanaume mmoja aliyekuwa akiimba nyimbo mbalimbali zinazoashiria kusindikiza uganga. Kuna wakati mganga alipokuwa akiendelea kupaka dawa, alifika kwenye eneo la kifua na mara baada ya kupaka, mrembo huyo aligeuka kumtazama mtu ambaye alikuwa akishuhudia tukio hilo (hakuonekana kwenye video).
MAONI YA WADAU
Video hiyo ilivyoshika kasi mitandaoni, watu mbalimbali walianza kutoa maoni yao huku kila mmoja akieleza lake bila kuwa na ushahidi wala uhakika wa wanachokisema. Kuna ambao walidai kuwa video hiyo imevujishwa na mchepuko wa mume wake Samirata lakini wengine wakadai si mchepuko bali ni mumewe.
NAKAYA ATAJWA
Kwenye maoni hayo, wapo waliomlaumu Nakaaya kuwa chanzo cha kuvuja kwa video hiyo wakidai alifanya hivyo makusudi kwa sababu aliwahi kumuuzia vipodozi Samirata kisha ‘akamzima’.Samirata atafutwa
Kufuatia video hiyo kuwa gumzo, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Samirata ambapo namba yake ilipopatikana, alipigiwa lakini alipokea mtu mwingine na kudai, mhusika hakuwa kwenye wakati mzuri wa kuongea.
HUYU HAPA NAKAAYA
Juzi, Risasi Jumamosi lilimtafuta Nakaaya kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu madai ya yeye kuwa chanzo cha kuvuja kwa video hiyo ambapo alisema si kweli bali yeye aliposti kama walivyoposti wengine.
“Mimi niliiposti tu kama wengine walivyoposti na kusindikiza na ujumbe wa kuwataka watu wafanye kazi waache ushirikina,” alisema Nakaaya.
Alipoulizwa kuhusu kufahamiana na Samirata na madai ya kwamba aliwahi kumuuzia mrembo huyo vipodozi kisha kuingia mitini, Nakaaya alisema huwa anamsikiasikia lakini hana uhusiano naye wa karibu. “Sina uhusiano naye na wala sijawahi kumuuzia vipodozi kama watu walivyosema mitandaoni,” alimaliza Nakaaya.
STORI: Boniphace Ngumije, Risasi Jumamosi
Comments are closed.