The House of Favourite Newspapers

Mitambo Mitatu ya Mabao Simba Kuikosa Polisi Tanzania Leo

0

KIUNGO wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck Rarry Bwalya leo ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

 

Kwa mujibu wa Vandenbroeck ni kwamba nyota huyo amepata matatizo ya kifamilia hivyo ataukosa mchezo wa leo jumlajumla.

 

Bwalya ndani ya Simba amehusika kwenye mabao mawili kati ya 29 yaliyofungwa msimu wa 2020/21 ambapo alisababisha faulo moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina Uwanja wa Mkapa ilifungwa na Pascal Wawa.

 

Mchezo huo ulikamilika kwa Simba kufunga mabao 3-0 na pasi yake ya bao alitoa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania.

 

Mbali na Bwalya pia kuna hatihati ya kumkosa beki wa kati Joash Onyango mwenye bao moja ndani ya ligi ambaye alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Plateau United.

 

Mwingine ni mshambuliaji, Chris Mugalu mwenye mabao matatu ambaye naye alikuwa anasumbuliwa na majeraha licha ya kuanza mazoezi, Vandenbroeck amesema kuwa nyota hawa uhakika ni kuanza kucheza Jumapili na sio leo. Jumla mabao sita leo yanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

 

Leave A Reply