Jana Februari 20, 2019, Rais Dkt. John Magufuli alikutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Dkt. Willem Jacobs, Ikulu jijini Dar, ambaye aliahidi kutekeleza ahadi ya malipo ya shilingi bilioni 682.5 kwa Serikali ya Tanzania kama walivyokubaliana mwaka 2017. Barrick yenye hisa nyingi (asilimia 63.9) ndani ya Acacia , ilikubaliana mambo matatu ikiwemo kutekeleza makubaliano ya kuendesha uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kutoa mgawanyo wa mapato ya kiuchumi wa asilimia 50 kwa 50 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya mtendaji huyo kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Kampuni ya Acacia wametoa taarifa wakikana kupokea mapendekezo yoyote kutoka kwa Barrick kuhusiana makubaliano yake na Serikali ya Tanzania hivyo kuwaweka Watanzania njiapanda kama watapata fedha hizo au la!
Je, nini maoni yako?


Comments are closed.