The House of Favourite Newspapers

MJADALA MZITO UMEIBUKA: LISSU VS NDUGAI, MTANDAONI PACHAFUKA!

MJADALA HOT: TUNDU LISSU Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amefanya ziara barani Ulaya na Marekani na kuisema Serikali. Wapinzani wake wanadai ameichafua nchi na wengine kuwa na shaka kwamba anasema hivyo kwa kuwa hatarejea nchini, licha ya kusema atarejea na ikiwezekana kugombea urais 2020.

 

Lissu amevituhumu vyombo vya dola akidai kuwa mpaka sasa hakuna aliyekamatwa wala kuhojiwa kutokana na kushambuliwa kwake licha ya polisi kuomba kumhoji wakati akitibiwa Nairobi, Kenya. Akihojiwa na VoA nchini Marekani jana, Balozi Wilson Masilingi alikanusha kashfa za Mbunge huyo kwa Serikali.

 

Spika Ndugai amesema atasimamisha mshahara wa Lissu kwa sababu hayupo bungeni, jimboni kwake wala hospitalini na spika hana taarifa za daktari. Nini maoni yako juu ya hili la LISSU? Tafadhali changia kwa hoja usitukane!

 

Nini maoni yako juu ya hili la LISSU, SPIKA NDUGAI NA SERIKALI?

Tafadhali changia kwa hoja usitukane!

Comments are closed.