The House of Favourite Newspapers

‘Mjamzito’ Anaswa Akisafirisha Madawa, Wanafunzi Wakutwa na Mirungi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata watu wanne kwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilogramu 18 mkoani humo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi na ni kosa la jinai.
Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Mwanza inasema, mtuhumiwa wa kwanza ambaye ni Bi. Frola Mwita (40), mkazi wa Tarime alikamatwa maeneo ya Nyakato akiwa na mirungi kiasi cha Kilogramu 8, alizokuwa amezifunga tumboni kwa seal tape na kuonekana kama mjamzito akiisafirisha kwa basi la Zacharia lenye namba T.569 CAP kutoka Tarime kwenda Mwanza.
Aidha, juzi Desemba 9, 2018 majira ya saa 2:00 usiku, jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba katika Mtaa wa Mahina a Wilayani Nyamagana yupo mtu anayefanya biashara hiyo jambo ambalo Polisi walifanya upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na kilogramu 10 za mirungi.
Watuhumiwa hao waliokamatwa ni;
  1. Saad Saba Kapinga, miaka, 49, mkazi wa Mahina
  2. Fatiha Saba, miaka 15, mwanafunzi wa kidato cha tatu Thaqaafa Secondary.
  3. Karen Saba, miaka 13, mwanafunzi wa kidato cha pili Musabe Secondary.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema linaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote wa nne pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.
Pia msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wa mtaa Mahina ambao wametoroka bado unaendelea. Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunaendelea na msako na ukaguzi wa magari yote yanayoingia Jijini Mwanza kutoka maeneo mbalimbali.
 
Katika tukio la Pili
Jeshi la Polisi Mkoani humo limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 27 kutoka nchi ya DRC –CONGO, walioingia nchini bila kibali wakipitia katika Kivuko cha Busisi /Kigongo Ferry, Wilayani Sengerema, kitendo ambacho ni kosa la Jinai.
Operesheni hiyo kabambe ya kukamata wahamiaji haramu imefanyika Desemba, 2018 majira ya saa 4:00 usiku. Imeelezwa kuwa wakati askari wakiendelea na doria pamoja na msako mkali katika kivuko cha Busisi ndipo walipokea taarifa toka kwa wasiri kwamba lipo gari kivukoni hapo limebeba wahamiaji haramu.
Baada ya kupokea taarifa hizo, Polisi walifanya msako mkali  pamoja na ukaguzi wa magari yote yaliyokuwepo kivukoni hapo na kufanikiwa  kuwakamata wahamiaji hao 27 wakiwa ndani ya gari wakielekea Jijini Mwanza, kati yao wanaume ni 15 na wanawake ni 12.
Wahamiaji hao haramu wamefahamika   kwa majina yafuatayo;
  1. Luganga Feruzi, miaka 40, toka jimbo la Kivu ya kusini Nchini DRC –Congo.
  2. Maria Ramadhani, miaka 30,  toka Jimbo la Kivu ya kusini Nchini DRC –Congo.
  3. Hamis  Luganga, miaka 12, mwanafunzi wa darasa la sita, Nchini DRC –Congo
  4. Hatia Lugunga, miaka  5, toka Nchi DRC –Congo
  5. Kyala  Lugunga, miaka  09 mwanafunzi wa darasa la tatu Nchini DRC- Congo
  6. Byaombe  Lugunga,mwanafunzi wa darasa la kwanza Nchini DRC –Congo
  7. Wilonja  Lugunga, miaka 5, toka Nchini DRC –Congo
  8. Ramadhan  Lugunga , miaka 3, toka Nchini DRC- Congo
  9.  Wilonja  Etungano, miaka 35, toka Kivu ya Kusini Nchini DRC – Congo
  10. Mitamba Ilonja, miaka 33, toka Kivu ya kusini Nchini DRC –Congo
  11. Byaombe Wilonja, miaka 16, mwanafunzi wa darasa la nne Nchini DRC- Congo
  12. Jilibeye Wilonja, miaka 13, mwanafunzi wa darasa la pili Nchini DRC –Congo.
  13. Mwenge Wilonja , miaka 12, Mwanafunzi wa darasa la nne Nchini DRC –Congo.
  14. Lucia Wilonja, miaka 10, mwanafunzi wa darasa la pili Nchini DRC –Congo.
  15. Joro Wilonja, miaka 8, mwanafunzi wa darasa la kwanza Nchini DRC –Congo.
  16. Shansi Wilonja, miaka 4, toka Nchini DRC – Congo
  17. Saidi Wilonja, miaka  2, toka Nchini DRC- Congo.
  18. Mbekalu  Asikulu, miaka 31, toka jimbo la Kivu ya Kusini Nchini DRC –Congo.
  19. Hamis Venance, miaka 30, toka jimbo la kivu ya Kusini Nchini DRC –Congo
  20. Maselina Mwibelecha, miaka 23, toka jimbo la Kivu ya Kusini Nchini DRC – Congo.
  21. Kashindi Hussein, miaka 3, toka jimbo la Kivu ya kusini Nchini DRC – Congo.
  22. Salive Hussein, mwaka 1, toka Nchini DRC –Congo.
  23. Regina Maua, miaka 28, toka  Jimbo la Kivu ya Kusini Nchini DRC –Congo.
  24. Debora Jamali, miaka 12, mwanafunzi wa darasa la nne Nchini DRC –Congo.
  25. Joseph Jamali, miaka 8, mwanafunzi wa darasa la pili Nchini DRC –Congo.
  26. Malekesa Jamali, miaka 5, toka Nchini DRC –Congo.
  27.  Jackson Jamali, miaka 2, toka Nchini DRC –Congo.

Wahamiaji Haramu Walivyonasa kwenye 18 za Polisi!

Aidha sababu za wahamiaji hao haramu kukimbia Nchini mwao DRC –Congo bado hazijafahamika. Jeshi wanaendelea na uchunguzi pamoja na mahojiano na wahamiaji hao haramu ili kuweza kufahamu sababu zilizowafanya kukimbia Nchi yao ya DRC –Congo na kubaini mbinu walizotumia kuingia Tanzania bila ya kukamatwa hadi kufika Mwanza. Aidha pindi uchunguzi ukikamilika wahamiaji hao haramu watakabidhiwa Idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi.
Jeshi hilo linatoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kuwa waache kwani ni kosa la Jinai na endapo mtu atabainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Sambamba na hilo, polisi wanawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwapa taarifa za wakimbizi/wahamiaji haramu wanaongia Nchini bila kufuata sheria ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Amber Rutty Alivyotinga Mahakamani na Mchungaji!

Comments are closed.