Mjue Miss Ufaransa, Mrembo wa Mbappe

ALICIA Aylies, mwanamitindo na Miss Ufaransa 2017 ambaye pia ni mpenzi wa straika staa wa PSG, Kylian Mbappe, amejiachia kwenye mitandao ya kijamii akionyesha alivyopiga picha na watu maarufu.

 

Picha hizo zinaonyesha kwamba mrembo huyo anafahamiana na watu kibao maarufu.

 

Picha ya kwanza ilimuonyesha akiwa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, nyingine zinaonyesha akiwa na muigizaji Tom Cruise, mrembo Flora Coquerel, mwimbaji Line Renaud na Vai Chaves ambaye ni Miss Ufaransa 2019.

 

Mrembo huyo aliyezaliwa Aprili 1998, amepiga kitabu akiwa na Digrii ya Sheria. Alicia amekuwa mdau mkubwa wa soka na amekuwa akipenda kushangilia timu ya Ufaransa na ile ya ‘bwana’ wake, Mbappe.


Loading...

Toa comment