The House of Favourite Newspapers

Mjumbe wa Bodi Simba: Mo Dewji Anataka Pesa alizozitoa kusadia Klabu zijumuishwe kwenye hisa

0

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba upande wa Wanachama CPA Issa Masoud amefunguka akidai Mwekezaji wa Simba Mohamed Dewji Mo amegeuza pesa za msaada anazotoa ndio Bilioni 20 anazotakiwa kuweka ndani ya Simba.

Akizungumza na waandishi wa habari usiku wa kuamia leo Juni 9, 2024, Masoud amesema walipokea taarifa ambazo hazikuwa katika urasmi wake ikiwataka kama bodi kupitisha azimio lililokuwa likisema pesa alizokuwa anazitoa mwekezaji kama msaada zihesabiwe katika hisa.

“Fedha zote ambazo MO alikuwa anazitoa yaani za kununua mchicha, kununua kandambili n.k za wachezaji zozote zile ambazo ametoa kwenye Simba Sports Club anazidai, na ameelekeza zibadilishwe ndio ziwe mtaji wake ambao anatakiwa autoe Simba Sports Club. Kama tunakopeswa hizo hela kwani lazima tukope kwa MO? Taasisi za fedha si zipo nyingi tunaweza tukakopa? Kwanza kama ni mkopo haujafuata taratibu alikopa nani na kwanini walikopa, na mkopo huo unawekwa kwa ajili ya aseti ipi ? amesema Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba upande wa Wanachama CPA Issa Masoud 

Leave A Reply