Mkandarasi Barabara ya Biafla Atakiwa Kuripoti Polisi – Video

  Mkandarasi alijenga barabara ya kiwango ya lami Biafla Kinondoni jijini Dar es Salaam ametakiwa kuripoti Polisi, siku ya Ijumaa kwa ajili ya kujieleza ni kwa nini asirudie Barabara hiyo anayodaiwa kuijenga chini ya kiwango.

Kauli hiyo ya kumtaka mkandarasi huyo kuripoti Polisi imetolewa leo Aprili 16, 2019, na RC Makonda wakati akiwa katika ziara yake Wilaya ya Kinondoni ambapo alikuwa akikagua miundombinu ya barabara na vituo vya afya vinavyojengwa kwenye wilaya hiyo.

Akielezea ziara yake, Makonda amesema anafurahishwa na miradi mbalimbali inavyoendelea vizuri huku akikemea baadhi ya wakandarasi wanaojenga miundombinu chini ya kiwango mfano wa barabara ya Barafu iliyopo Mburahati ambayo mkandarasi ametakiwa Kurudia mifereji aliyoijenga chini ya kiwango ya kupitishia maji.

Katika ziara hiyo aliweza pia kutembelea soko la Africa Sana na Soko la Magomeni ambapo yote kwa pamoja alifurahishwa na maendeleo yanayoendelea ya ujenzi wa masoko hayo.

TAZAMA VIDEO HII

Loading...

Toa comment