The House of Favourite Newspapers

Mkapa, Mangula, Mwenyekiti UVCCM Wamtembelea Magufuli Ikulu – Pichaz

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa (kushoto) pamoja na Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Philip Mangula Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

 

Rais Magufuli akijadiliana jambo na mzee Mkapa (kulia) pamoja na Mangula (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mndolwa, Kabaka pamoja na Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Magufuli akiagana na Herry James mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka

 

Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana(UVCCM) Herry James Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

 

Comments are closed.