The House of Favourite Newspapers

Mkataba wa Aukus: Marekani, Uingereza, na Australia Zakubaliana Kuhusu Mradi wa Nyuklia wa Manowari

0

Viongozi wa Marekani, Uingereza na Australia wamefichua maelezo mapyaya mpango wao wa kubuni manoari ya kizazi kipya inayotumia nishati ya nyuklia .

Chini ya makubaliano ya Aukus Australia itapokea kwanza walau manoari tatu zinazotumia nishati ya nyuklia kutoka kwa Marekani.

Washirika hao pia watashirikiana kwa pamoja kubuni manoari mpya ya kiteknolojia, mkiwemo vinu vya nyuklia vilivyotengenezwa na kampuni ya Rolls-Royce ya nchini Uingereza.

Makataba huo unalenga kukabiliana na ushawishi wa Uchina katika kanda ya bahari ya India na ile ya Pacific.

Akizungumza na viongozi wengine mjini San Diego, California, Rais wa Marekani Joe Biden alisisitza kwamba maboti hayatakuwa na silaha za nyuklia na hayatabadilisha sera ya Austaralia ya kuwa nchi isiyokuwa na nyuklia .

Chini ya mkataba ulioainishwa Jumatatu , wanajeshi wa majini wa kikosi cha Australia – Royal Australian Navy (RAN) watafanya kazi na vikosi vya Marekani na Uingereza.

DC JOKATE NDANI ya TAMASHA KUBWA LA UREMBO, VAZI LA STARA, WAANZILISHI WAFUNGUKA…

Leave A Reply