The House of Favourite Newspapers

Mkataba wa Mromania wa Azam Upo Tayari

0

Said Ally|CHAMPIONI|GPL

UONGOZI wa timu ya Azam utamsainisha kocha wake, Aristica Cioaba mkataba mpya wa kuifundisha timu hiyo muda mfupi tu baada ya kurejea kutoka Arusha ambako wamealikwa kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki pamoja na kwenda kutoa pole kwa waliofikwa na msiba wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Lucky Vincent.
Aristica aliyechukua mikoba ya Mhispania, Zeben Hernandez, mkataba wake umemalizika punde tu baada ya ligi kufika ukingoni ambapo alisaini mktaba wa miezi sita wa kuinoa timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, ameliambia Championi Jumatatu kuwa tayari wameshaandaa mkataba kwa ajili ya kocha huyo na wameshakubaliana kila kitu ambapo kilichobaki kwa sasa ni kutia saini ambayo itakamilishwa baada ya kurejea kutoka Arusha. “Kocha wetu amemaliza
mkataba wake lakini tayari tumeshamuandalia mkataba mpya ambao tunatagemea atasaini muda mfupi baada ya timu kutoka Arusha ambako tumealikwa na timu za huko. “Tunampa mkataba huo baada ya kuridhishwa na kazi yake ambayo ameifanya ndani ya muda mfupi ambao amekaa na sisi na tunaamini kama tukiendelea kukaa naye, tuna uwezo wa kufika mbali zaidi ya tulipomaliza kwenye msimu huu.
“Lakini pia tumechoka tabia ya kubadilibadili makocha ambayo ilituponza msimu uliopita na kujikuta tukiangukia katika nafasi mbaya kwani tuliwachanganya wachezaji wetu baada ya kuwabadilishia falsafa za walimu wawili kwa wakati mmoja,” alisema Kawemba.

Leave A Reply