The House of Favourite Newspapers

Mkate wa Maboga, Nazi na Maziwa

LEO tutaona jinsi ya kupika mkate wa maboga, nazi na maziwa.

MAHITAJI

Unga wa ngano kilo 1

Hamira kijiko 1

Chumvi ½ kijiko cha chai

Sukari kijiko 1

Maziwa ,tui bubu la nazi

Uji mzito wa maboga yaliyochemshwa na kupoa kikombe 1

Vanila nusu ½ kijiko

Siagi kidogo.

 

KUANDAA NA KUPIKA

Andaa maji ya uvuguvugu nusu kikombe kidogo cha chai.

Weka hamira kwenye hayo maji ya uvuguvugu kisha funika kwa muda wa dakika 4 hadi 5.

Andaa unga wa ngano, chekecha ili kutoa uchafu (kama una mchanyiko na vitu tofauti)

Pasha moto sufuria ya kukandia.

Chemsha mafuta ya kula. Mimina hamira (ambayo tayari imeumuka kwenye maji) kwenye unga.

Changanya vizuri kisha mimina mchanganyiko kwenye mafuta yanayochemka.

Koroga kwa kutumia mwiko, japokuwa ni vizuri sana ukitumia mkono (kuwa makini mafuta yasiwe ya moto sana.)

 

Ongeza maziwa au tui la nazi na endelea kukanda hadi unga uwe laini na usigandiane na sufuria.

Weka siagi kidogo kisha endelea kukanda.

Changanya vanilla kisha endelea kukanda.

Ukimaliza kukanda vizuri, paka sufuria mafuta, weka mchanganyiko wa unga uliokanda kisha funika, weka sehemu yenye uvuguvugu au joto kwa dakika 30 mpaka 45 ili unga uumuke vizuri.

 

Joto liwe kati ya nyuzi 80°C hadi 120°C.

Kama unatumia oven ni vizuri kama utawasha ili lipate moto kabla ya kuweka mchanganyiko wa unga.

Zima kabla ya kuweka mchanganyiko wako. Kisha weka mchanganyiko ili uumuke vizuri.

Kwenye jiko la mkaa linatakiwa kuwa na moto mdogo kiasi.

Mchanganyiko wa unga wenye hamira ukishaumuka vizuri, kanda tena kiasi na kisha gawa matonge madogomadogo (kutokana na umbo utakalo).

Panga matonge kwenye mduara wa sufuria ambao umepaka mafuta au siagi kisha weka kwenye sehemu yenye joto au vuguvugu kwa muda dakika 45. Joto liwe kati ya nyuzi 80°C hadi 120°C.

 

Angalia kama unga umeumuka vizuri na kuongezeka kwenye sufuria.

Weka moto kwenye jiko la mkaa ili liwe la moto kwa dakika 10 .

Punguza moto na injika sufuria yenye matonge yako juu ya jiko.

Palia mkaa wenye jivu la moto juu ya mfuniko na subiri kwa dakika 10 kisha funua uangalie kama zimeiva.

 

Kama bado ongeza moto wa jivu kidogo kisha subiri kwa dakika tano.

Ukifunua na kuona zimebadilika rangi na kuwa kahawia zipake siagi kwa juu kisha funika tena.

Baada ya dakika mbili mimina matonge yako kwenye chombo kisafi acha yapoe.

Yakishapoa hapo yapo tayari kwa kula. Unaweza kula na chai, maziwa, kahawa au vinywaji tofauti.

 

Gladness Mallya |  MAPISHI YA LEO!

Comments are closed.