The House of Favourite Newspapers

Mke adai kuchomwa visu na mumewe!

mke-achomwa-visu-7 Stori: Mayasa Mariwata, Gazeti la Ijumaa Wikienda, Toleo la Januari 2, 2017

Dar es Salaam: Majanga kuelekea Mwaka Mpya 2017! Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mwanamke aliyeomba kujitambulisha kwa jina moja la Judith (pichani juu) aliyedai kunusa kifo baada ya kuchomwa visu na mumewe kisha kuchoma moto nyumba.

mke-achomwa-visu-8Judith akionesha majeraha kichwani

Unalikumbuka tukio la nyumba kuungua moto maeneo ya Sinza-Mugabe, Dar, Jumatano iliyopita, majira ya saa saba mchana? Nyumba hiyo inadaiwa kuchomwa na mwanaume aliyetajwa na Judith kuwa mumewe, muda mfupi baada ya kumfanyia ukatili wa kutisha walikokuwa wakiishi Mbezi-Beach jijini Dar.

mke-achomwa-visu-4Majirani wakitoa mabaki ya vitu baada ya nyumba kuteketezwa kwa moto.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza na Ijumaa Wikienda wakati likiwa kwenye uchunguzi wa tukio hilo, jamaa huyo alidaiwa kufika kwenye nyumba hiyo na kuonekana akizunguka huku na kule.

mke-achomwa-visu-3Namna nyumba hiyo ilivyoungua.

Ilidaiwa kwamba, katika kuzunguka kwake alikuwa akiimwagia petroli nyumba hiyo kabla ya kuiwasha moto na kutoweka kusikojulikana.

“Yule mume wa Da Judith alifika hapa, akamwambia mwenzetu mmoja atuambie wapangaji wenzake kuwa tusilipe kodi kwa sababu nyumba itavunjwa kumbe alikuwa na mipango yake ya kuichoma moto kwa lengo la kumkomoa mkewe kwa sababu hawakai kwenye nyumba hii ila Judith ana pub (grosari) yake hapa.

mke-achomwa-visu-1“Ndani ya nyumba iliyoungua kulikuwa na fremu zetu, vitu vingi vimeungua, tumepata hasara kubwa kisha yeye amekimbia mpaka sasa hatujui alipo.

“Kama alikuwa na ugomvi na mkewe si wangeyamaliza tu maana tunasikia amemjeruhi yupo taaban,” alisema mmoja wa waathirika huku wenzake wakimsapoti.

Kufuatia ishu hiyo, paparazi wetu alimtafuta Judith ambapo alifanikiwa kumuona akiwa na majeraha kwa madai kuwa alichomwa visu na mumewe huyo maeneo mbalimbali ya mwili wake Siku ya Krismasi akiwa nyumbani kwake maeneo ya Mbezi-Beach.

mke-achomwa-visu-5Judith aliliambia Wikienda kuwa, tukio hilo limemsikitisha mno: “Huyu mwanaume nina miaka mitatu naye, mwanzo tuliachana kwa sababu ya kunipiga mara kwa mara, lakini nikajua amejirekebisha tukayamaliza, ile Siku ya Krismasi alinipiga sana na kunichoma visu kichwani na mikononi. “Pia alivunja madirisha ya nyumba yangu ya Mbezi-Beach kisha akakimbia.

“Nilijikokotota hadi hospitali maana Mbezi-Beach tunapoishi kumepoa, sikupata wa kunisaidia kwani simu zangu pia aliondoka nazo.

mke-achomwa-visu-6“Jumatano iliyopita ndipo nikapewa taarifa kuwa alifanya tukio hilo la kuunguza pub yangu ili kunikomoa maana hiyo nyumba ya Sinza-Mugabe nilipewa na baba yangu, ya Mbezi-Beach nimejenga mwenyewe, nashindwa hata kwenda eneo la tukio maana bado sipo vizuri kiafya kutokana na kipigo na nahisi nitakufa kwa presha.”

Aliendelea kusimulia kuwa, anachotaka mwanaume huyo akamatwe na kufikishwa kituo cha polisi na yupo tayari kumpa fedha mtu atakayemkamatisha kwani kwa unyama aliomfanyia siku ya sikukuu, haamini kama yupo hai hadi sasa.mke-achomwa-visu-2

Kufuatia sekeseke hilo la kupigwa, Judith alifungua kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe, Dar, kwa jalada la kesi namba KW/RB/15018/2016 –KUJERUHI na ishu ya moto alifungua kwenye Kituo cha Polisi cha Urafiki, Ubungo kwa jalada namba  URP/RB/11733/2016- KUCHOMEWA NYUMBA MOTO ambapo hadi Wikienda linakwenda mitamboni jana, mwanaume huyo alikuwa akisakwa na polisi.

back-wikienda

Gazeti la Ijumaa Wikienda, Toleo la Januari 1, 2017

Comments are closed.