The House of Favourite Newspapers

Mke, mchepuko wagombea maiti!

0

Mke wa marehemu, Anna.

Dustan Shekidele, Moro

Kha! Mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Bella aliyedaiwa kuwa ‘mchepuko’ wa mwanaume aitwaye Lugano aliyefariki dunia wiki iliyopita, alinusurika kipigo baada ya kuvamia msibani akigombea maiti na mke wa ndoa.

Tukio hilo la kushangaza lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri wiki iliyopita nyumbani kwa marehemu huyo maeneo ya Kota za Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (Sua) mjini hapa.Katika purukushani hiyo, kulizuka makundi mawili ambapo kundi la mke wa ndoa lilimsapoti mke wa marehemu na lingine lilimsapoti Bella hivyo kusababisha msiba kuwa uwanja wa vita.

Mchepuko unaodaiwa kugombea maiti.

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Ashura aliyekuwa upande wa Bella alimng’ata sikio mwandishi wetu: “Ninachojua ni kwamba Lugano alikuwa anatembea na Bella na kwa bahati mbaya aliugua, cha ajabu mke wa ndoa alimtelekeza hivyo Bella akabeba jukumu la kumuuguza hadi anafikwa na umauti.

Kwa upande wa waliokuwa wanamsapoti mke wa ndoa walidai Bella hakuwa na soni kwenda msibani nyumbani kwa mke wa ndoa na zaidi sana alitaka tu kuleta shari.

Akizungumza na gazeti hili, mke wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Anna alidai kwamba alisikitishwa na kitendo cha mwanamke huyo kumfanyia fujo ambapo Bella aliondolewa pale msibani akiwa chini ya ulinzi mkali.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply