The House of Favourite Newspapers

Mke wa Dk. Slaa Ala Bata Hatari USA

0

MKE WA DRJosephine Mushumbusi, mke wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Peter Slaa akiwa USA.

Josephine Mushumbusi, mke wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Peter Slaa anadaiwa kula bata za hatari nchini Marekani (United States of Amerika au U.S.A) akiwa na familia yake, Amani limenyaka maisha yake nyuma ya pazia.

Ishu hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu Josephine alipoibua gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo baada ya kuanikwa mambo yake ya siri na Askofu wa Kanisa na Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akimtuhumu kumteka mumewe, Dk. Slaa na kumshawishi kuachana na siasa.

ANASWA SEHEMU AKIJIDAI

Kwa mujibu wa Wabongo waishio nchini humo (Diaspora), Josephine aliyetua nchini humo siku kadhaa zilizopita akitokea Bongo na familia yake, amekuwa akinaswa sehemu mbalimbali akijidai na kujiachia kwa raha zake.

“Mwacheni atulize machungu na maumivu jamani. Kusema kweli amehangaika sana na Chadema na siasa za Tanzania hivyo ameona bora ajiachie,” kilisema moja kati ya vyanzo vyetu na kuongeza:

“Nafikiri huyu mama (Josephine) anaondoa stress (mawazo) ya Gwajima na machungu ya kukosa u-first lady (mke wa rais) baada ya mumewe (Dk. Slaa) kukosa nafasi ya kugombea urais ambayo Chadema walimpa Edward Lowassa baada ya kujiunga na chama hicho.”

BATA MWANZO-MWISHO

Habari zilieleza kwamba, mwanzoni mwanamama huyo alidaiwa kuonekana akila bata na kujiachia na rafiki zake katika Jimbo la Maryland kabla ya kutimkia Indiana na wamekuwa hawatulii jimbo moja kwani wameonekana pia huko Minnesota nchini Marekani.

“Unajua wana marafiki kwenye majimbo mbalimbali hivyo hawatulii sehemu moja,” kilidai chanzo chetu.

MSIKIE JOSEPHINE

Akizungumza na gazeti moja nchini (siyo la Global) akiwa nchini humo juu ya maisha yake kwa sasa, Josephine alikaririwa akisema:

“You will see my fruits (utayaona mafanikio yangu). For the time being my hands are closed (kwa sasa nimefunga mikono yangu).

“Niruhusuni niendelee na maisha ya siasa nje ya siasa. Majungu, propaganda nawaachia wahusika…sijaona issue (jambo) lolote lenye content (maudhui) ya kujibu alichozungumza Gwajima.

“Am very busy now (sina nafasi kwa sasa). And life is demanding too (na maisha yananihitaji pia), why should I waste time with things which are not adding any value to me? Thank you. (Kwanini nipoteze muda kwa vitu ambavyo haviniongezei thamani yoyote? Asante).”

NINI KIFUATACHO?

Kwa mujibu wa Josephine, kwa sasa yeye na Dk. Slaa wapo mapumzikoni nchini humo lakini wanajipanga kwa upande mwingine wa kuwa wawekezaji na uwekezaji waliopanga baada ya kupewa fedha na marafiki zao ni kujenga shule, hospitali na kuwawezesha wanawake wajasiriamali pindi watakaporejea Bongo kutoka Marekani.

Leave A Reply