The House of Favourite Newspapers

Mke wa kigogo apagawa jumba lake kuvunjwa!

0

IMG_1068

Akiwa haamini anachokiona.

Deogratius Mongela na Chande Abdallah
MSHTUKO! Mama mmoja mke wa kigogo mfanyabiashara, aliyetajwa kwa jina moja la Catherine, mkazi wa Mbezi Beach Libermann jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipagawa vibaya wakati jumba lake la thamani likivunjwa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni waliokuwa wakipewa ulinzi mkali na polisi.

Mwanamke huyo, alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya nyumba yake inayodaiwa kuwa na thamani ya shilingi Milioni 500 kuvunjwa kwenye zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam.

Katika eneo la tukio, gazeti hili lilimshuhudia mke huyo akionekana kuchanganyikiwa, akiwasihi maofisa wa halmashauri hiyo kuacha kutekeleza kusudio lao, kwani suala la nyumba hiyo lilikuwa mahakamani, jambo ambalo lilipingwa na zoezi hilo kuendelea bila pingamizi.

IMG_1070

Akikwepa kupigwa picha.

Akiwa haamini kilichoendelea, mama huyo alichukua dumu la maji lenye ujazo wa lita tano na kuanza kuzunguka nalo huku na huko, akinywa maji na kuzungumza kwa simu na ndugu zake wa karibu, kiasi cha kuwashangaza mashuhuda, waliojiuliza kwa nini hakuchukua chupa ndogo ya lita moja!

Inadaiwa kuwa mume wa mama huyo aliyetajwa kwa jina moja la Deusdedith, alivamia kiwanja hicho Block J 712 zaidi ya miaka 10 iliyopita na baada ya mmiliki wake halali, Protax Bilali kwenda mahakamani, alishinda kesi lakini mvamizi huyo alikaidi amri ya kuondoka eneo hilo hadi sheria ilipochukua mkondo wake wiki iliyopita.

IMG_1098Mama huyo alisikika akimpigia simu mumewe ambaye inadaiwa wakati huo alikuwa mahakamani akijitahidi kupata zuio la utekelezaji wa zoezi hilo. Kwa mujibu wa mazungumzo yao, mume huyo alimweleza mkewe kuwa alikuwa anawasiliana na vigogo serikalini ili kusitisha shughuli hiyo.

IMG_1086Ubomoaji ukiendelea.

“Mama amesema mumewe amempigia (jina linahifadhiwa, la mtoto wa rais mstaafu) lakini akamwambia yeye hawezi kumsaidia, labda ampigie kigogo wa ardhi ambaye pia amemwambia zoezi hilo ni gumu kwa sasa, mama amepagawa kabisa,” alisema shuhuda mmoja mbele ya gazeti hili.

Katika kipindi cha siku tatu, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imevunja jumla ya nyumba 26 zilizojengwa katika maeneo ya wazi na yaliyovamiwa na kwa mujibu wa Injinia Baraka Mkuya wa manispaa hiyo, zoezi hilo litaendelea baada ya wiki mbili.

Leave A Reply