The House of Favourite Newspapers

Mke wa Kobe Awashtaki Waliosababisha Kifo cha Mumewe

0

VANESSA BRYANT ameishtaki Kampuni ya Island Express na rubani wa helikopta iliyopata ajali na kusababisha kifo cha mumewe, bintiye na watu wengine saba. Amesema hali ya hewa haikuwa salama kwa safari na helikopta ilikuwa mbovu, hivyo ametaka kulipwa fidia kwa kupoteza wapendwa wake.

Miongoni mwa mashtaka dhidi ya kampuni hiyo ni kwamba safari hiyo ilifanywa wakati ukungu ulikuwa ni mwingi kwa chini na hivyo kusababisha rubani asiweze kuona vizuri, jambo lililosababisha helikopta hiyo ianguke huko Calabasas, California.

 

Mbali na Vanessa kutaka fidia za mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kupoteza upendo uliokuwapo na watu hao wa familia yake, matunzo, furaha, huduma na kadhalika, anataka pia kufidiwa gharama za mazishi ya watu hao.

Leave A Reply