The House of Favourite Newspapers

Mke wa Mtu Afanyiwa Kitu Mbaya Mwezi Mtukufu

0
Sunday Kisesa (aliyetapeliwa)

 

DAR ES SALAAM: WAKATI Waislamu ulimwenguni kote wakiwa kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, wengine wameonekana kuendeleza matukio ya uharifu ambapo Jeshi la Polisi Dar linamshikilia mwanamme aliyefahamika kwa jina la Rajabu Juma Gafu kwa tuhuma za kumtapeli mwanamke aliyefahamika kwa jina la Sunday Kisesa mkazi wa Morogoro.

 

Akielezea sakata hilo kwa wanahabari wetu, Sunday alisema yeye ni mfanyabiashara mwenye maskani yake Morogoro Mjini lakini mara nyingi huwa anakuja Dar kufuata mzigo wa biashara.

 

“Hivi karibuni nikiwa mitaa ya Kariakoo natafuta bidhaa alitokea kaka flani akiwa na uso wa tabasamu mbele yangu kama vile mtu aliyenifahamu nami nikashawishika kumsikiliza maana huwezi kumpuuza mtu huenda akawa anakufahamu kweli nawe ulimsahau.

 

Nilipoanza kumsalimia alionekana alipata data nyingi za ukweli zinazonihusu maana alianza kunikumbushia maisha ya kule Morogoro tangu nikiwa nasoma naye alisema eti tusoma shule moja.

Rajabu Juma Gafu (mtuhumiwa wa utapeli)

 

Aliongea mambo mengi ambayo yalinifanya nione nimekutana na ndugu ambaye si wa kumpuuza.

Baada ya maongezi aliniuliza ninakokwenda baada ya kumaliza kufungasha mzigo nikamwambia nakwenda Ubungo Terminal kupanda basi nirudi Morogoro.

 

Nilipomwambia hivyo akanionesha gari yake na kuniambia hata yeye alikuwa akielekea maeneo ya Ubungo hivyo ingekuwa vizuri anisindikize mpaka hapo nikapande basi.

 

“Niliona ni njambo la heri lakini safari ilipoanza aliniomba tupitie Sinza sikuweza kumpinga tulienda mpaka Baa moja maarufu akasimamisha gari na kuniambia ilikuwa ni mapema mno na kuniomba tupate juisi.

 

Nilipokunywa ile juisi baada ya muda nikaanza kusikia macho na mdomo vinakuwa vizito haraka kabla sijaanza kulewa vizuri aliniingiza kwenye gari lake yake na kuniambia nimtajie namba yangu ya siri ya benki akatoe pesa ili anipeleke hospitali vinginevyo ningeweza kufa.

 

Kwakuwa nilikuwa katika hali ya kutojitambua vizuri nikajikuta nampa namba yangu ya kutolea pesa kwenye kadi ya benki ambapo alifanikiwa kutoa shilingi milioni mbili, simu tatu za kisasa Smart phone, randi 800 za Afrika Kusini, cheni ya dhahabu raba pea tatu na mkoba wenye vitu vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni nne.” Alisema mwanamke huyo.

 

Baada ya kunifanyia hayo alikwenda kunitelekeza kwenye baa ya Hongera iliyopo Sinza ambapo nilipopata fahamu nilikwenda kufungua kesi kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama kwenye jalada namba KIN/RB/5017/2017.

 

Nashukuru Mungu baada ya kutoa ripoti na kufungua kesi hiyo polisi walifanya jitihada na kumtia mbaroni mtuhumiwa ambapo taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.

Waandishi wetu

 

Breaking News: Rais Magufuli Azindua Mradi wa Maji Ruvu Juu, Amtaka Mkurugenzi Dawasa Ajiondoe

Leave A Reply