The House of Favourite Newspapers

MKE WA RAIS BUSH AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 92

MKE wa rais wa 41 wa Marekani, George H W Bush, ambaye pia ni mama wa rais wa zamani wa Marekani, George W Bush, Barbara Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

 

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na Ofisi ya Rais George H W Bush na ilieleza kifo chake kimetokana na matatizo ya kiafya ambapo mara kadhaa mama Bush alilazwa hospitalini na siku ya Jumapili aliamua abakie nyumbani akiwa na familia yake.

 

Januari mwaka 2017, yeye na mumewe rais mstaafu Bush walilazwa kwa wakati mmoja. Yeye alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya koo, huku mumewe akitibiwa kwa ugonjwa wa nyumonia.

 

Mama Bush ni mmoja kati wanawake wawili tu nchini Marekani, kuwahi kuwa mke wa rais na mama wa rais. Abigail Adams alikuwa mke wa John Adams, na mama wa rais John Quincy Adams, rais wa sita wa Marekani.

Comments are closed.