The House of Favourite Newspapers

Mke wa rais wa Zanzibar katika ziara ya kuwaombea kura wagombea wa ccm

0

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Mfenesini Unguja wakati akiwa katika ziara yake kuwatembelea Viongozi wa Wanawake Zanzibar kuwapigia kampeni Wagombea wa CCM kwa Wananchi kupitia Wanawake.

Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume amewataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kukipigia Kura Chama cha Mapinduzi ili kukipatia ushindi wa kishindo na kusisitiza wasipoteze kura zao wakati wao Mwanake alikuwa haruhusiwi kupiga kura wakati wa ukoloni.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif akizungumza na Wanawake wa Wilaya ya Mfenesini Unguja na kuwataka kutumia nafasi zao kutowa elimu kwa wananchi kuhamasika kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya tarehe 25/10/2015.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mama Asha Balozi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na Wanawake wa Wilaya ya Mfenesini Unguja kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura kwa Wagombea wa CCM.

Mgombea Uwakilishi Jimbo la Bububu Masoud Abdurahaman akiomba kura na kuwaombea kura Wagombea wote wa CCM na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.

Mgombea Ubunge Jimbo la Mfenesini kwa tiketi ya CCM Kanali Mstaaf Masoud akiomba kura kwa Viongozi wa UWT waliohidhuria mkutano wa Mama Mwanamwema Shein, kuwaombea kura Wagombea Urais wa Zanzibar na Tanzania kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein na Dk John Pombe Magufuli.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Welezo Mhe Saada Mkuya, akiomba kura kwa Viongozi wa UWT wakati wa mkutano na Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Malimu Nyerere Bububu Zanzibar.

Wanachama wa CCM Jumuiya ya UWT wakimshangilia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wakati akiwatambulisha Wagombea Ubunge na Uwakilishi wa Wilaya ya Mfenesini Unguja wakati wa mkutano wake uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu Zanzibar.

Viongozi wa UWT Wilaya ya Mfenesini Unguja wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia na kuwaomba kura kuwapigia Wagombea wote wa CCM.

Leave A Reply