The House of Favourite Newspapers

Mke wa TB Joshua Amrithi Mumewe

0

MKE  wa aliyekuwa mhubiri maarufu Nigeria, TB Joshua, Nabii Everlyn Joshua ameteuliwa kuwa kiongozi wa kanisa Sinagogi kwa mataifa yote, taarifa ya kanisa hilo imesema sasa litakuwa chini ya Nabii Everlyn chini ya uongozi wa Mungu.

 

Awali kulikuwa na maswali ya kujua nani atakabidhiwa kanisa kuliongoza mara baada ya mwasisi TB Joshua kufariki dunia ghafla Mei mwaka huu jijini Lagos.

 

Nabii Evelyn Joshua alizaliwa tarehe 17 Disemba 1968 katika eneo la Okala Okpumo, Jimbo la Delta nchini , Nigeria, kwa wazazi wake Bwana na Bibi Nicholas Akobundo kwa hivyo basi mwezi Juni, 2021 Evelyn Joshua ametimiza umri wa miaka 52.

 

Evelyn Joshua amekuwa Muhimili katika maisha ya mumewe na huduma yake ya kanisa japo alionekana nadra sana kando ya mumewe wakati wa mahubiri ya mikusanyiko ya watu , Bi Evelyn ndiye alikuwa Mkuu wa pili wa kanisa hilo ambalo kwa Kingereza linaitwa  The Synagogue, Church of All Nations, na anasemekana amechangia pakubwa katika shughuli za huduma na maendeleo ya kanisa hilo.

 

Evelyn Joshua anaaminiwa kuwa ndiye mtu wa pili mwenye ushawishi zaidi katika kanisa la Synagogue baada ya mume wake. Mara kwa mara amekuwa akikutana na kuwapa ushauri nasaha watu binafsi ambao hawakuweza kukutana na TB Joshua enzi za uhai wake  pia huhubiri kanisani.

 

Evelyne alikutana na Temitope Balogun Joshua wakati alipokuwa katika kazi zake na baadaye akawa mtu maarufu. Mnamo mwaka 1990, Evelyn alisafiri katika eneo la Egbe kumtembelea dada yake, wakati alipokuwa huko alikutana na Mchungaji TB Joshua, ambaye alimzidi umri kwa miaka mitano.

 

Alikuwa amekwenda kukutana naye kwa ajili ya kupata ushauri nasaha na muongozo wa kiroho  na mkutano wao ambao ulidumu kwa muda wa dakika arobaini na tano, ulikua chanzo cha safari yao ya ndoa.

 

Kulingana na marehemu nabii TB Joshua, kukutana na mke wake kulipangwa na Mungu, na alimuomba amuoe siku hiyo hiyo.

 

Evelyn alikuwa na hofu juu ya ombi la ndoa ambayo haijui, licha ya kwamba alisema ndio, na wakaoana na kuishi katika ndoa kwa miaka 30.

Ndoa ya nabii TB Joshua na Evelyn Joshua ilizaa matunda, kwani waliweza kupata watoto watatu.

Leave A Reply