The House of Favourite Newspapers

Mke wa Zamani wa Donald Trump, Ivana Afariki Dunia Akiwa na Umri wa Miaka 73

0
MKE wa kwanza wa  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, Ivana Trump ambaye amefariki dunia Julai 14, 2022

MKE wa kwanza wa  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, Ivana Trump amefariki dunia Julai 14, 2022 nyumbani kwake  jijini New York akiwa na umri wa miaka 73.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Donald Trump kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii unaojulikana kama Truth Social aliandika   “Ninayo huzuni kubwa kuwafahamisha wote mliompenda,  kwamba Ivana Trump amefariki dunia nyumbani kwake jijini New York.

 

Alikuwa ni mwanamke mzuri na wa ajabu, ambaye aliishi maisha mazuri na daima fahari na furaha yake kubwa walikuwa ni watoto wake watatu, Donald Jr., Ivanka, na Eric, alijivunia sana wao , kwani sote tulijivunia yeye. Pumzika kwa Amani, Ivana”

 

Ivana alikuwa ni mke wa kwanza wa Donald Trump ambapo walifunga ndoa yao mnamo mwaka 1977 na kufanikiwa kupata watoto watatu ambao ni Donald Jr, Ivanka na Eric kabla ya ndoa kuvunjika na kupelekea kuachana kwao mnamo mwaka 1992.

 

Leave A Reply