The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mkemi Akiri ubingwa Bado Mgumu Yanga

0

LICHA ya kubakiwa na mechi tatu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Salum Mkemi amefunguka bado wapo katika wakati mgumu wa kutetea ubingwa wao kutokana na kucheza mechi mgumu mfululizo.

 Yanga  yenye pointi 62 sawa na Simba inayokamata nafasi pili   inaongoza ligi kwa  wastani wa mabao ya kufungwa huku  kitakiwa kucheza mechi zake  tatu zilibaki ndani ya siku  wiki moja. Kesho Jumamosi Yanga inacheza na Mbeya City kisha Toto African kabla ya kuelekea Mwanza kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya Mbao FC.

Kutoka kushoto ni wachambuzi, Wilbert Molandi, Philip Nkini, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Salum Mkemi, Mchambuzi na Mhariri Kiongozi wa Gazeti la Championi, Saleh Ally.

Akizungumza katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha Spoti Hausi kinachorushwa na Global TV kila Alhamisi saa 10:00 Jioni, Mkemi alisema kuwa kazi iliyobaki kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa msimu ni kubwa kutokana na mechi zao kufuatana mfululizo.

“Bado ubingwa gumu ukiangalia ligi namna ambayo inavyoenda kwa sababu tuna mechi tatu na zote ngumu, tunacheza na Mbeya City, Toto African, Jumanne halafu Jumamosi tunatakiwa tumalize na Mbao kule Mwanza.

 “Sasa hapo unaona ugumu ambao upo kwa sababu jirani zetu wao wanaombea tuteleze tu lakini sisi kwetu tunazitaka hizo pointi tisa kwa nguvu zote maana timu ipo kwenye kiwango kizuri,” alisema Mkemi.   

 

Leave A Reply