The House of Favourite Newspapers

Mkeo anakosa hamu ya tendo la ndoa? msaidie hivi

0

Ni Jumanne nyingine ninapokukaribisha mpenzi msomaji wangu katika uwanja wetu huu mzuri. Karibu tena kwenye ukurasa huu murua tujuzane mambo mbalimbali yahusuyo sanaa ya mapenzi na maisha.

Tunaendelea kuidadavua mada yetu tuliyoanza nayo wiki iliyopita juu ya namna ya kumsaidia mkeo anaposumbuliwa na tatizo la kupoteza hamu ya tendo la ndoa.

Tuliangalia kwa kina juu ya sababu zinazomfanya mwanamke akakosa hamu ya tendo la ndoa, tukachambua dalili za tatizo hilo na mwisho tukaanza kuelezea nini cha kufanya ili kumsaidia mwenzi wako anayesumbuliwa na tatizo hilo.

Nakushukuru wewe msomaji wangu uliyewasiliana nami na kutoa maoni yako lakini kikubwa nilichokibaini ni kwamba, ukiachana na wanawake ambao ndiyo husumbuliwa mara kwa mara na tatizo hili, wengi wamelalamika kwamba hata wanaume pia wanasumbuliwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Kitu cha kwanza tulichoeleza wiki iliyopita ili kumsaidia mkeo anayepoteza hamu ya tendo ni kushughulikia migogoro ya kimapenzi inayowakabili. Mbinu nyingine tuliona ni kumsaidia mkeo kupambana na tatizo la msongo wa mawazo. Leo tunaendelea na mbinu nyingine:

3. MRIDHISHE MUWAPO FARAGHA
Sababu nyingine inayosababisha mwanamke kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwenzi wake ni mwanaume kushindwa kumridhisha wanapokuwa faragha.

Narudia tena kusema kwamba mapenzi ni kama sanaa nyingine yoyote ambayo ni lazima ujifunze ili uwe hodari. Huwezi kujua kupiga gitaa na likatoa muziki mzuri kama hukujifunza, vivyo hivyo kwenye mapenzi.

Wanaume wengi wana tatizo la kushindwa kuwafikisha wenzi wao wawapo faragha na kwa bahati mbaya zaidi, wengi hawapo tayari kujifunza. Wanaishi kwa mazoea, wanashiriki tendo kwa namna ileile, hakuna ubunifu, hakuna kujifunza na matokeo yake, wanasababisha wenzi wao wakose msisimko wa kuendelea kushiriki nao.

Ndiyo! Atafurahia vipi kuwa na wewe faragha wakati anajua kwamba utamuacha njiani baada ya kumaliza haja zako na hutashughulika kwa chochote kuhakikisha na yeye anafurahi?

Ni muhimu kwa wanaume kujifunza namna ya kuwafurahisha wenzi wao wawapo faragha ili kudumisha uhusiano imara. Ni matumaini yangu kwamba mpaka hapo, wanaume watakuwa wamepata kitu cha kujifunza.

4. MFANYIE MAMBO MAZURI
Mbinu nyingine ya kumsaidia mkeo kama amepoteza hamu ya tendo ni kuwa na utaratibu wa kumfanyia mambo mazuri. Wanandoa wengi wakishaoana, wanaona kama wameshamaliza kila kitu. Wanaacha kufanya yale mambo yote waliyokuwa wanayafanya awali ambayo ndiyo yaliyosababisha wenzi wao wakawapenda.

Mfanyie ‘sapraizi’ mkeo kwa kumnunulia zawadi mara kwa mara, hata kama ni ndogo kiasi gani.

Tenga muda wa kuwa naye hata kama ratiba zako zinakubana kiasi gani na pale unapopata muda, mtoe ‘out’. Mambo haya japo unaweza kuyaona kama ni madogo, lakini husaidia kwa kiasi kikubwa kuamsha upya hisia za mapenzi.

Leave A Reply