TANGU mwaka 2005, Kanisa la Victory Christian Center chini ya Mchungaji Dr Huruma Nkone limekuwa likiandaa mkesha mkubwa wa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu, sasa habari njema ni kwamba la safari hii litakuwa balaa kwani limesheheni!
Tamasha hilo linahusisha burudani na mafundisho yanayomsaidia kijana kuwa raia mwema katika nchi yake na kuongeza ufahamu wake wa maisha. Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa matamasha haya, mwaka huu tamasha hili linafanyika mara mbili.
Lilifanyika Aprili, mwaka huu kwa mafanikio makubwa na wanafunzi kutoka pande zote za Dar na mikoa ya jirani walihudhuria.
Leo Ijumaa kwa baraka zote za Mungu pamoja na kibali cha Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, tamasha hilo linafanyika tena palepale kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar kuanzia saa moja kamili usiku.
Kutakuwa na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania kama vile Mkhululi Bhebhe kutoka Afrika Kusini, Joel Lwaga (Tanzania) na Beda Andrew (Tanzania).
Wengine ni Upendo Nkone (Tanzania), Mshindi wa Bongo Star Search (BSS) 2012, Walter Chilambo, Rivers of International, Zabron Choir, The Voice na Hype Square.
Kwa upande wa wazungumzaji kwa vijana, atakuwepo mhasisi wa matamasha haya, Dr Huruma Nkone, Eric Shigongo na Sam Sasali na pia tutakuwa na ugeni maalum wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.
Ni siku ambayo kijana na mwanafunzi wa Jiji la Dar hatakiwi kukosa!
“Ni siku ambayo kijana atajifunza, lakini wakati huohuo atapata burudani na pia kupata ujumbe mzuri wa nyimbo za dini kutoka kwa waimbaji nguli wa gospo,” alisema Shigongo alipokuwa akilielezea tamasha hilo.
Comments are closed.