Mkhului Bhebhe KukiwashaTena Campus Night – Dar – Video

KWA MARA NYINGINE TENA KATIKA VIWANJA vya Tanganyika Packers – Kawe, jijini Dar es Salaam, patakuwa hapatoshi Ijumaa ijayo, Novemba 15, 2019, kwani patakuwa na Tamasha la Kimataifa na la kihistoria litakalofanyika kuwaunganisha wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini na nje ya nchi, watumishi wa Mungu na watu wote wenye kupenda kulijua neno la Mungu.

Victory Campus Night 2019, ambalo limeandaliwa na Kanisa la VCCT – Mbezi Beach, chini ya mchungaji Dkt. Huruma Nkone, hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu kutakuwa na sapraizi nyingi zaidi zitakazokuinua na kukufanya uwe wa tofauti.


Kutakuwa na maombi, kusifu, kuabudu, mafundisho mbalimbali ya neno la Mungu na nasaha kutoka kwa wahamasishaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi akiwemo Eric Shigongo, zitakazokupa mbinu za kujikwamua.

Tayari mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili kutoka nchini Zimbabwe, Mkhuhuli Bhebhe, anayetamba na wimbo ujulikanao kama Ndiyeyu Jesu Medley, ndiye atakayeongoza jahazi la burudani kwenye tamasha hilo.

Mbali na Mchungaji, Dr. Huruma Nkone na Eric Shigongo, wengine watakaounguruma jukwaani hapo ni pamoja na mtangazaji wa Clouds Media, Samuel Sasali, Masanja Mkandamizaji.

Pia watakuwepo wasanii kibao kutoka kiwanda cha nyimbo za Injili hapa nchini akiwemo Masanja Mkandamizaji, Upendo Nkone, Dr. Ipyana Kibona, Joel  Lwaga, TCG Dance, Winners of Students Audition, Wlater Chilambo na wengine wengi.

Bila kumsahau Mkuu wa Mkoa wa dar es salaam, paul makonda pia atakuwepo kufanya maombi, Mkuu wa Wilaya ya handeni, Godwin Gondwe na wengine wengi. Usithubutu kuikosa hii historia ya aian yake.

TAZAMA SHOO YA MKHULULI BHEBHE


Loading...

Toa comment