The House of Favourite Newspapers

Mkhululi Bhebhe Asepa na Kijiji Tamasha la Campus Night – Video

MUIMBAJI maarufu wa muziki wa Injili raia wa Zimbabwe ambaye anaishi nchini Afrika Kusini, Mkhululi Bhebhe amefanya maajabu wakati akitumbuiza kwenye Kongamano la Victory Campus Night la mwaka 2019, ambalo limefanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers usiku wa leo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu waliofika kwa ajili ya kumshukuru Mungu na kukutana na marafiki.

Mkhululi ambaye alishangiliwa na jukwaa zima wakati akipanda jukwaani kutumbuiza ameonyesha umahili mkubwa na kudhihirisha kuwa kweli ni mwimbaji wa Kimataifa baada ya kuangusha burudani ya aina yake jambo ambalo liliwaamsha mashabiki wake wote na kuanza kuimba nyimbo zake mwanzo hadi mwisho huku wakicheza na kushangilia kwa kusifu.

 

Mkhululi alioyekuwa akisubiliwa kwa hamu na Watanzania kupanda jukwaani, aliimba nyimbo zake tatu kali ikiwemo Ichokwadi na Zvamaronga.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Kanisa la VCCT – Mbezi Beach, chini ya mchungaji Dkt. Huruma Nkone limetikisa Jiji la Dar es Salaam licha ya mvua kunyesha lakini watu walijaa uwanjani na ratiba ikaenda kama ilivyokuwa imepangwa.

 

Katika tamasha hilo, ambalo limeanza majira ya saa 1:00 jioni, waimbaji mbalimbali wamepanda jukwaani kuimba wakimsifu Mungu baadhi yao ni, Upendo Nkone, AIC Chang’ombe Kwaya, Joel Lwaga, Walter Chilambo na wengine wengi.

 

PICHA NA: RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.