Mkongo Awamaliza Mastaa

MwamiPedeshee Mkongo, Rajab Mwami

Mwandishi wetu
Pedeshee Mkongo anayefahamika kwa jina la Rajab Mwami, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwenye maskani jijini Dar, amegandwa na madai ya kutaka kuwamaliza mastaa wa kike Bongo kutokana na kuwa na uhusiano nao kwa nyakati tofauti.

wolper[1]Jacqueline Wolper

Madai hayo yanakuja kufuatia jamaa huyo awali kuripotiwa kuwa na uhusiano na staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe kabla ya baadaye kuhamia kwa Video Queen, Husna Maulid.

luluuuElizabeth Michael ‘Lulu’

AMTAKA LULU
Habari ya mjini ni kwamba, baada ya kutokea hali ya kutokuelewana kati ya Wolper na Husna, jamaa huyo aliamua kuachana nao na baadaye akatangaza kuwa, yuko tayari kupoteza kiasi chochote cha fedha ilimradi amnase staa mwingine wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja kama alifanikiwa kutimiza azma yake hiyo kwani kilipita kimya kidogo bila kujulikana anatoka na staa gani.

wema3Wema Sepetu

ADAIWA KUMNASA WEMA
Baada ya kupita kimya kirefu, yaliibuka madai kuwa, Mkongo huyo amejiweka kwa mwigizaji Wema Sepetu na kwamba kufuru alizokuwa akifanya mwandada huyo mjini, zilitokana na jeuri ya fedha za Mwami.

tunda-21.jpgTunda Sabasita

ATUA KWA TUNDA
Kana kwamba jamaa huyo hatulii kwa demu mmoja, kuna kipindi yaliibuka tena madai kuwa amejiweka kwa Video Queen wa Bongo, Tunda Sabasita hali iliyosababisha watu kuhoji sababu ya mabinti hao kumpapatikia.

shamsaaaaShamsa Ford

SHAMSA ADAI KUTOKEWA
Naye staa mwingine wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford aliwahi kunukuliwa na gazeti hili akidai kuwa, Mkongo aliyewahi kuwa na Wema na Wolper, amemtokea.
Hata hivyo, hakukuwa na ushahidi kama aliyemtokea ni Mwami au Mkongo mwingine ambaye huenda aliwahi kuwatokea Wema na Wolper.

MASOGANGE5Agness Gerald ‘Masogange’

MASOGANGE NAYE KABANG
Wakati watu wakihisi jamaa huyo katulia zake Kongo, juzikati Mkongo huyo akanaswa akiwa na Video Queen mwingine wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ wakiwa hotelini na akadai wapo kibiashara zaidi.

Hata baada ya pedeshee huyo kujitetea, wengi walidai kuwa, licha ya uwezekano wa kuwepo kwa biashara kati ya wawili hao, kwa jinsi anavyopenda watoto wazuri, hawezi kumuacha.

HOFU YA KUAMBUKIZANA UKIMWI YATANDA
Kufuatia mastaa hao kupishana kwa pedeshee huyo, wengi waliozungumza na Ijumaa walionesha hofu yao ya kuambukizana ugonjwa hatari wa Ukimwi.

“Yaani huyu jamaa sijui pesa zake ndiyo zinampa kiburi, maana kila staa anayemtaka anamtokea, lakini hofu yangu ni kwamba kama anatembea nao wote bila kinga si watakuwa wanaambukizana?” alihoji Husna Juma wa Kinondoni huku akiomba ikiwezekana jamaa huyo arudishwe kwao kwani atawamaliza mastaa hao.

MWAMI ANASEMAJE?
Baada ya kuwepo kwa msururu ‘mtungo’ huo wa mastaa wakiwepo aliowapitia na aliopanga kuwapitia, mwandishi wetu alimtafuta Mwami kupitia simu yake ya mkononi ambapo katika kujitetea alisema kuwa, yeye ni mtu na familia yake na hao mastaa wengi wao wanajigonga kwake.

“Hao bwana wanajigonga kutokana na tamaa zao, mimi siwezi kuwa nao kwa kuwa nina mke wangu na nampenda sana,” alisema Mwami.


Loading...

Toa comment