The House of Favourite Newspapers

Mkude Aibuka Simba Baada ya Siku 60

0

KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude, ameubukia ndani ya kikosi cha timu hiyo baada ya kukosekana kwa takribani siku 60 kutokana na kusimamishwa na kamati ya nidhamu ya klabu hiyo.

 

Desemba 28, mwaka jana, Simba ilitangaza kumsimamisha Mkude kwa kosa la kinidhamu, ambapo tangu hapo, alikosekana kwenye mechi 14, kabla ya juzi Ijumaa kuibuka na kucheza dakika zote tisini katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la FA dhidi ya African Lyon na Simba kushinda 3-0.

Wakati Mkude akiwa nje ya uwanja, Simba katika mechi 14, ilifunga mabao 31 na kuruhusu sita ndani ya dakika 1260.

Mechi hizo ni; Simba 5-0 Majimaji, Simba 4-0 Ihefu, Simba 4-0 FC Platinum, Simba 3-1 Chipukizi, Simba 2-0 Mtibwa Sugar, Simba 2-1 Namungo na Yanga 0-0 Simba (Yanga ikashinda kwa penalti 4-3).

 

Zingine ni; Simba 4-1 Al Hilal, Simba 0-0 TP Mazembe, Dodoma Jiji 1-2 Simba, Biashara United 0-1 Simba, Simba 2-2 Azam FC, AS Vita 0-1 Simba na Simba 1-0 Al Ahly.

STORI NA LUNYAMDZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply