NA MWANDISHI WETU |CHAMPIONI
NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amesema leo Jumamosi wataingia uwanjani kwa nia moja tu ya kushinda na kutwaa ubingwa wa Kombe la FA na wala hawatafanya mzaha kwa wapinzani wao, Mbao FC.
Simba na Mbao ya Mwanza, leo Jumamosi zinapambana kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani hapa katika mechi ya fainali ya Kombe la FA.
Mkude ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kikosi chao kina ari nzuri na matarajio yao ni kucheza bila ya kuwadharau wapinzani wao jambo ambalo litawafanya washinde kirahisi.
“Ni wazi fainali yoyote ile lazima iwe ngumu na sijawahi kuona fainali nyepesi kabla ya kuchezwa, hivyo mchezo wetu na Mbao utakuwa mgumu na wala si mwepesi kama watu wanavyodhani.
“Wao wamejiandaa na sisi tumejiandaa, lakini niwaombe mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani kutupa sapoti kwani nao wana mchango katika timu.
“Mbao ni timu nzuri, ukiangalia walipotoka mpaka wamefika hapa wamefanya kazi kubwa, hivyo hatuwezi kuwadharau hata kidogo, tutaingia uwanjani kwa ajili ya ushindi tu,” alisema Mkude.