The House of Favourite Newspapers

Mkude Kama Ajib, Ajiandaa Kutimkia Nje

mkudeNahodha wa Simba, Jonas Mkude naye yupo njiani kutimka klabuni hapo na kwenda kutafuta maisha nje ya nchi kama alivyofanya Ibrahim Ajibu ambaye sasa yupo nchini Misri.
Ajibu anatafuta nafasi ya kucheza soka la kulipwa katika Klabu ya Haras El Hodood ambapo tayari amefuzu vipimo vya afya na kilichobakia ili aweze kujiunga na timu hiyo ni endapo benchi la ufundi litavutiwa na uwezo wake uwanjani.
Mmoja wa marafiki wa Mkude amesema wakala wa Mkude hivi sasa yupo katika harakati za kumtafutia mchezaji huyo timu nje ya nchini ikiwa ni siku chache tu baada ya uongozi wa Simba kumkabidhi mkataba mpya.
“Mkataba mpya ameshauona lakini inawezekana asiusaini kwani wakala wake yupo katika harakati za kumtafutia timu nje ya nchi na jinsi mambo yanavyoelekea, anaweza kuondoka nchini muda wowote.
“Anaweza kwenda Misri au Algeria au nchi nyingine za Kiarabu zilizopo nje ya Afrika pia kuna timu Vietnam, huko atafanya majaribio na akifuzu atajiunga na timu mojawapo,” alisema rafiki huyo.
Alipotafutwa Mkude mwenyewe kuhusiana na ishu hiyo alisema: “Mimi bado ni mchezaji wa Simba na wakala wangu hajaniambia jambo lolote kuhusu dili hilo.
“Wakala wangu hivi karibuni alikuja nchini kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Krisimasi, atakaponiambia kuhusu kwenda kufanya majaribio nitasema kila kitu.”

Mkataba wa Mkude na Simba unamalizika Januari, mwakani lakini mpaka sasa hajasaini mwingine mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo licha ya kupewa mkataba huo.
SOURCE: CHAMPIONI

Comments are closed.