The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mkude: Kila Anayekuja Mbele Yetu Tunamfyatua

Mkude (Kushoto) akiwa na Awadhi

Na SAID ALLY|CHAMPIONI JUMAMOSI| HABARI

NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude amesema kwamba hawaihofii timu yoyote watakayokutana nayo mbele yao na dhamira yao ni kukifunga kikosi chochote watakachokutana nacho.

Kauli hiyo ya Mkude imekuja baada ya Simba kufanya vizuri katika mechi zake tatu ambapo mbili ni za Ligi Kuu Bara na moja ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la FA. Simba imezifunga Majimaji (3-0) na Prisons kwa idadi kama hiyo ya mabao katika mechi za ligi kuu halafu ikaifunga African Lyon bao 1-0 katika Kombe la FA.

Jonas Mkude

Simba ambao wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 51, Februari 25, mwaka huu watacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mkude ameliambia Championi Jumamosi kuwa, wao wamejiwekea lengo la kushinda mechi zao tisa zilizobakia bila ya kuangalia aina gani ya timu wanayokutana nayo.

“Muhimu kwa sasa ni kushinda tu hakuna jambo lingine kwa ajili ya kutimiza kile tulichokianza tangu mwanzoni mwa msimu huu ambacho ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa ligi kuu.

“Haitajalisha nani tunacheza naye bali kikubwa ni kushinda pekee na hilo tunataka kulitimiza kwenye mechi hizi tisa zilizobakia kama ambavyo tumekuwa tukishinda katika mechi nyingine,” alisema Mkude

Comments are closed.