The House of Favourite Newspapers

Mkude, Morrison Out Leo Kuwakosa Kagera Sugar Uwanja wa Mkapa, Ligi Kuu

0
Bernard Morrison.

 

WAKATI leo kikosi cha Simba kikiwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar, nyota wake wanne wanatarajiwa kukosa mchezo kutokana na sababu mbalimbali.

 

Nyota hao wa Simba watakaokosa mechi ya leo pale Uwanja wa Mkapa, Dar, Jonas Mkude Tadeo Lwanga, Sadio Kanoute na Bernard Morrison ambao hawako fiti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco alisema: “Morrison ni majeruhi ipo hivyo kwa Kanoute, Lwanga na Mkude hawatakuwa sehemu ya kikosi kwa sababu bado hawajawa fiti ila wapo wachezaji wengine ambao tumewaandaa kwa ajili ya mchezo huo hasa katika eneo la kiungo.

“Tutakuja na kitu cha tofauti katika maeneo yote ili kuweza kupata matokeo na tunajua ni timu imara kwa kuwa tuliwahi kukutana nao hivyo kuanzia eneo la ulinzi na kiungo tutakuwa tofauti ili kupata pointi tatu ambazo tunazihitaji kwa ajili ya kuwa katika nafasi nzuri ya kupata ubingwa kwani ligi bado haijaisha.

 

“Tumefanyia kazi eneo la mapigo huru, utaona kwenye mechi yetu iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting tuliweza kufunga kwa mapigo huru hivyo tunazidi kuimarika katika hilo, mashabiki wajitokeze kupata burudani.”

 

Naye Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Buberwa Birikesi alisema: “Tunajua tunaenda kucheza na timu yenye mashabiki wengi lakini tumejipanga vizuri kwa mbinu mbalimbali ili kuweza kuondoka na pointi tatu na hakuna majeruhi hata mmoja wachezaji wetu wako vizuri kupambana na Simba.”

Waandishi: Lunyamadzo Mlyuka, Angela Mmbaga, Silvia Chalamila na Kilima Mohamedi.

Waandishi Wetu

#​​BREAKING: MBOWE ANATANGAZA RASMI HATMA YA HALIMA MDEE NA WENZAKE MUDA HUU..

Leave A Reply