The House of Favourite Newspapers

Mkude: Tulieni Pointi Tatu za Singida Zinakuja

BAADA ya Simba kutokuwa na matokeo mazuri katika mechi za hivi karibuni kwa kutolewa kwenye Kombe la FA na Mapinduzi katika hatua ya makundi, kiungo wa Simba, Jonas Mkude amewapoza mashabiki wa timu hiyo kwa kusema watachukua pointi tatu za Singida United.

Simba inatarajiwa kuvaana na Singida United siku ya Alhamisi jijini Dar kuwania pointi tatu katika mchezo unaotabiriwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na kiwango cha timu zote mbili.

 

Simba inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 26 sawa na Azam FC wakiwa wanapishana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku Singida ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 23.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkude amesema kuwa, mchezo huo utakuwa na ushindani hivyo wanajipanga kupata pointi tatu.

 

“Mechi yetu na Singida itakuwa nzuri na tumejiandaa kwa ajili ya kupata pointi tatu kwani wapinzani wetu wapo vizuri na tunatarajia kukutana na upinzani mkubwa katika mchezo huo.

“Kikosi chetu kipo vizuri kuelekea katika mchezo huo, tumejipanga kufanya vyema kila mchezaji anahitaji kuisaidia timu kuweza kutwaa ubingwa,” alisema Mkude.

 Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.