Mkuki Moyoni Mwangu – 03
NI usiku, kuna kila aina ya kelele nje, kuanzia ngoma za vigodoro mpaka milio ya vyura, Kevin Mdoe yupo ndani ya kibanda kidogo kilichojengwa kwa madebe kando ya mto, karibu na dampo, maeneo ya Tandale Taptap, maarufu kwa uuzwaji wa pombe za kienyeji.
Kitandani amelala mkewe, Catarina, mgonjwa akiwa amebakiza mifupa na ngozi, huku mwili ukiwa umejaa vidonda vingi vinavyotoa harufu mbaya, yu katika hali ya kufa na hana fahamu! Ingawa chumba hakina umeme lakini kwa kutumia mwanga wa koroboi iliyomo chumbani mwao, Kevin anaziangalia picha za mke wake alizopiga wakati akiwa mrembo, mwenye afya njema kwenye mashindano ya uanamitindo sehemu mbalimbali za dunia ikiwemo Paris, London na New York.
Wote wawili hawakutarajia kwamba siku moja wangejikuta wakiishi katika maisha waliyokuwemo, dunia ilikuwa imewageuka, wa mwisho alikuwa mbele na wa mbele alikuwa mwisho! Machozi yalikuwa yakimbubujika Kevin akikumbuka jinsi yeye na mkewe walivyokutana miaka mingi kabla, baba yake alipohamishwa kutoka Tanga alikokuwa akifanya kazi kama Meneja wa Tanesco kuletwa Dar es Salaam ambako aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa shirika hilo kubwa.
Siku ya kwanza shuleni (Academic International School), akiwa na umri wa miaka saba ndiko alikutana na Catarina aliyekuwa na umri wa miaka mitano, wakisubiri kuchukuliwa na wazazi wao baada ya masomo, ghafla wakazoeana, baba yake alipomchukua ndani ya gari, Kevin alianza kumsimulia juu ya msichana mrembo aliyemwona shuleni! Badala ya kufurahi, baba yake alianza kumpa maonyo.
Historia hii inajirudia kichwani mwa Kevin, akiwa ndani ya chumba kilichotoa harufu kali ya mkewe, machozi yanamtoka na kudondoka kwenye sakafu ya udongo.
Je, nini kitaendelea?SONGA NAYO…
BABA yake Kevin, Joseph Mdoe na mkewe Davina Lema, walipanga nyumba maeneo ya Masaki kwenye nyumba nyingi zilizojengwa na shirika la nyumba la taifa na kupewa jina la Kijiji cha NHC Estate, humo ndimo wafanyakazi wengi wa mashirika ya serikali waliishi.
Wakati baba yake Kevin akiendesha gari kuelekea kwenye lango kuu la kuingia Kijiji cha NHC Estate, ghafla ilitokea gari nyeupe aina ya Land Cruiser V8, lililofanana kabisa na alilokuwa akiendesha, Kevin alipoliangalia gari hilo na baadaye kutupa macho ndani yake, alijikuta tu akipiga kelele mbele ya baba yake bila kuogopa.
“Dad! Dad! Look! That is the girl I was telling about!” (Baba! Baba! Angalia! Yule ndiye msichana niliyekuwa nakueleza habari zake!)
“Kevin! Can you zip your lips? I told you not to concentrate on girls at the moment!” (Kevin! Unaweza kufunga mdomo wako? Nimeshakuambia usiweke mawazo yako yote kwa wasichana!)
“No dad! I just wanted you to see her.” (Hapana baba! Nilitaka tu umwone.)
Baba yake hakuongea tena chochote, akakanyaga breki na kusubiri gari lililokuwa mbele yake liingie kwanza, hilo ndilo gari ambalo ndani yake alipanda Catarina ambaye pia alikuwa akihangaika kumwangalia Kevin na kutoa tabasamu zuri lakini mwenzake hakuitikia kwa sababu baba alishatoa angalizo.
Jambo ambalo hawakulitegemea, magari yote yalipoingia, Kevin alishangaa kuona gari lililombeba Catarina likiingia nyumba namba 32 na ya kwao ilikuwa namba 33! Zikiwa zimetenganishwa na uzio wa senyenge uliowezesha mtu wa nyumba moja kuona kilichoendelea upande wa pili.
Kevin alishuka garini macho yake yote yakiwa yamevuka ukuta wa senyenge kuelekea upande wa pili ambako alimshuhudia Catarina akishuka kwenye gari lao naye akili yake ikiwa imeishia upande wa pili, alinyanyua mkono wake na kumpungia Kevin huku akitabasamu lakini mwenzake hakujibu sababu baba alikuwa karibu.
“I can see your mind is not here with me!” (Naona akili yako yote haiko hapa na mimi!)
“Why?” (Kwa nini?)
“May be you should ask your eyes, to know what they have seen!” (Labda uyaulize macho yako yakueleze yalichokiona!)
“No dad! I am here with you, how can I be somewhere else?” (Hapana baba! Niko hapa nawe, nawezaje kuwa sehemu nyingine yoyote?)
Baba yake hakujibu kitu, wakaanza kutembea kuelekea ndani ya nyumba, hatua tatu tu mbele, Kevin aligeuka kuangalia nyuma baba yake akiwa amemshika mkono, alikuwa akimwangalia Catarina ambaye pia alitembea na baba yake kuelekea ndani ya nyumba.
Nyumba zote ndani ya eneo la Kijiji NHC Estate, zilifanana kwa muundo, hivyo baada ya kufika ndani na kumsalimia mama yake, Kevin alipandisha ngazi haraka kabla hata hajavua viatu na nguo za shule mpaka ghorofa ya kwanza kwenye veranda ya chumba chake, alipotokeza tu nje, alishangaa kumwona Catarina naye akiwa amesimama kwenye veranda yao, wote wakatabasamu.
“So you live here?” (Kwa hiyo unaishi hapa?) Kevin alimuuliza Catarina.
“Yes!” (ndiyo!)
“We just moved in few days ago!” (Tumehamia siku chache zilizopita!)
“My name is Catarina!” (Naitwa Catarina!)
“I am Kevi…!” (Naitwa Kevi…) hakuweza kumalizia sentensi yake baada ya kusikia maneno “Kevin where are you?” yaliyomaanisha kuuliza mahali alipokuwa, kwa kasi ya umeme alifungua mlango akaingia ndani ya chumba chake na kujitupa kitandani.
Baba yake alipoingia ndani alimkuta amejilaza na kitabu mkononi, kama vile alikuwa akisoma kwa bidii sana, kama kawaida ya wazazi aliketi kitandani na kuanza kumpa nasaha nyingi ambazo kwa Kevin ziliingilia upande huu na kutokea mwingine, kifupi alikuwa hajielewi wala kujitambua kwa Catarina, ingawa wote walikuwa ni watoto wadogo.
“Where were you?” (Ulikuwa wapi?) baba yake aliuliza.
“I was here revising my Math home work!” (Nilikuwa hapa nikirejea kazi yangu ya nyumbani ya Somo la Hesabu!)
“Kevin! You are lying!” (Kevin! Unanidanganya!)
“No dad!” (Hapana baba!)
“That girl is taking you off your rail!” (Huyo msichana anakupoteza njia!)
“I am sorry dad, it is just that, I can’t get her out of my mind.” (Samahani baba, yote hiyo ni kwa sababu siwezi kumwondoa kichwani mwangu!)
Hivyo ndivyo ilivyoanza, wakawa marafiki wakubwa, juhudi za wazazi wao kuwatenganisha ziligonga mwamba, ikabidi wazazi pia wawe marafiki wa karibu ambao mara nyingi mwisho wa wiki walikwenda pamoja nje ya mji kupumzika na familia zao, ilitokea tu familia zote mbili zikawa na mtoto mmojammoja!
Hakuna siku ambayo ilipita bila Kevin na Catarina kusimama kwenye veranda za nyumba zao na kuongea, hasa pale ambapo wazazi hawakuwepo nyumbani, kila mmoja alisimama kwenye veranda yao na kuongea maneno yote waliyotaka kuongea, Catarina akimwelezea Kevin nia yake ya kuwa mwanamitindo baadaye akikua.
“Why do you want to be a model?” (Kwa nini unataka kuwa mwanamitindo?)
“I just love it!” (Napenda tu!)
“Who is your role model?”(Mtu anayekuvutia kwenye fani hiyo ni nani?)
“Naomi Campbell!”
“Who is Naomi Campbell?” (Naomi Campbell ni nani?)
“An International super model, don’t you know her?” (Ni mwanamitindo wa kimataifa, humjui?)
“No! I am not a fashion person.” (Hapana! Mimi siyo mtu wa mitindo)
“Wait!” (Subiri!) alisema Catarina na kukimbia kuingia ndani ya nyumba yao, alipotokeza dakika tatu baadaye, alikuwa na picha kubwa ya mwanamitindo Naomi Campbell na kumwonyesha Kevin, akionyesha furaha yake.
“Oooh! Yeah! I know her, I just didn’t know her name is Naomi Campbell, so you want to be like her?” (Oooh! Ndiyo! Namjua, sikujua tu jina lake ni Naomi Campbell, kwa hiyo unataka kuwa kama yeye?)
“200%” (Asilimia mia mbili!)
“I wish you all the best!” (Nakutakia kila la kheri!)
“What about you? What do you want to be?” (Vipi kuhusu wewe? Unataka kuwa nani?)
“An engineer, but my father wants me to be a doctor!” (Nataka kuwa mhandisi, lakini baba yangu anataka niwe daktari!)
“Follow your heart, that is your dream not his!” (Fuata moyo wako, hiyo ni ndoto yako, siyo ya baba yako!)
“Do your parents support you in becoming model?” (Wazazi wako wanakuunga mkono kuwa mwanamitindo?)
“Yes!” (Ndiyo!)
Kevin aliendelea kukumbuka maisha yake ya nyuma kama vile alikuwa akiangalia sinema ya mapenzi, hakuwahi kuwaza kabisa kuwa maishani mwake angejikuta katika maisha ya dhiki kama aliyokuwa nayo, Catarina akiwa amelala kitandani hajitambui, mwili ukitoa harufu mbaya, asingeweza kumkimbia kwani alikuwa ni mke wake ambaye aliapa mbele ya Mchungaji kuwa angeishi naye maisha yote katika shida na raha.
JE, nini kitaendelea? Fuatilia kesho katika Gazeti la Championi Jumamosi.
Comments are closed.