Mkulima wa Manyara Aliyejishindia Gari na Magift ya Kugift Apelekewa Mpaka Kijijini Kwake
Ibrahim Njeja, mkulima kutoka Manyara, akipiga picha na mke wake baada ya kupokea gari aina ya Kia Seltos aliloshinda katika kampeni ya “Magift ya Kugift” huko Msitu wa Tembo, Manyara.
Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Kampuni ya Mtandao wa simu ya Yas ambapo wateja wake waliokuwa wakitumia mtandao huo kupata huduma mbalimbali walikuwa wakiingizwa kwenye droo ya bahati nasibu.
Kabla ya ushindi wa Ibrahim wateja wa kampuni hiyo wameshajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo za milioni 1, milioni 5, milioni 10, simu za mkononi na nyinginezo.
