The House of Favourite Newspapers

Mkulima wa Simanjiro Ajishindia Gari Jipya na Magift ya Kugift

Afisa Mkuu wa Mixx by Yas Bi Angelika Pesha akimkabidhi funguo za gari lake mkulima wa Simanjiro, Ibrahim Njema (mwenye fulana ya njano).

Akizungumza kwenye hafla ya kumkabidhi zawadi hiyo, Mkurugenzi wa Masoko, Kutoka Yas, Edwardina Mgendi, amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa mshindi huyo ambaye ni mkulima wa kawaida, jambo ambalo linathibitisha kuwa kampeni yao ni ya kweli na haki lakini pia yeyote anaweza kushinda inachotakiwa ni kufanya miamala na huduma nyinginezo za kampuni hiyo.

Afisa Mkuu wa Mixx by Yas Bi Angelika Pesha akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mgendi  amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milioni 400, kwa washindi wa makundi  tofauti ikiwemo, mawakala na wateja wengine.

Aidha Mgendi amesisitiza kuwa huu ni mwanzo tu kwani Yas Tanzania ina anaandaa promosheni nyingine baada kumalizika hii ya Magift ya Kugift.

Naye Afisa Mkuu wa Mixx by Yas, Angelika Pesha amesema mshindi huyo alipatikana katika droo maalum ambayo ilifanyika na hatimaye, Ibrahim Njema kuibuka na gari hilo la kisasa.

Kwa upande wake mshindi huyo ameishukuru Yas kwa kuendesha kampeni hiyo ambayo imemfanya aibuke na mshindi huo ambapo amewaomba Watanzania kuendelea kushiriki kampeni hiyo ikiwa sambamba na kutumia huduma za Yas, kwani na wao huenda wakawa washindi.