Mkurugenzi Halmashauri ya Msalala Anusurika Kifo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, Simon Berege na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mibako Mabubu wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kugonga ng’ombe usiku wa kuamkia leo katika eneo la Shelui, mteremko wa Mlima Sakenke mkoani Singida.

Viongozi hao walikuwa wakitokea mkoani Dodoma kuelekea Igunga, Tabora kuwahi kikao cha utekelezaji wa ilani ya CCM kitakachofanyika kesho Jumamosi Septemba 15, 2018.
Katika gari hilo, Mkurugenzi huyo  alikuwa pamoja na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, mweka hazina, Masatu Mnyoro na mwanasheria wake, Mashaka Mabula ambao wamelazwa katika Hospitali ya Igunga mkoani Tabora wakiendelea kupatiwa matibabu.
 
Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Bonaventura Kalumbete amesema  Berege na Mabula ndiyo waliokuwa wamelazwa lakini baada ya kuwapatia matibabu hali zao zinaendelea vizuri na wakati wowote wataruhusiwa.

 

Loading...

Toa comment