Mkurugenzi Mkuu WHO Atoa Pole kifo cha Dkt Faustine Ndugulile
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus ametuma salamu za pole Tanzania kufuatia kifo cha mkurugenzi mteule wa shirika hilo kanda ya Afrika, ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile.
Kupitia ukurasa wake wa X, Tedros Gabreyesus amechapisha ujumbe akisema ” nimeshtushwa na kuhuzunishwa sana kusikia kuhusu kifo cha ghafla cha Dk. Faustine Ndugulile, Mkurugenzi mteule wa kanda ya Afrika wa WHO.
“Pole zangu za dhati kwa familia yake, marafiki zake, Bunge na watu wa Tanzania”.
Dkt Faustine Ndugulile alichaguliwa rasmi nafasi ya Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Agosti 27 mwaka huu, akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Dr Matshidiso Moeti.
Dkt Faustine Ndugulile amefariki hii leo Novemba 27, huko nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.