Mkurugenzi Mtendaji Absa Bank Tanzania Aibuka Kidedea Tuzo za Watendaji Wakuu Bora 100

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser, ameibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya mshindi wa pili katika kipengele cha Mkurugenzi Mtendaji Bora wa Mwaka, katika Tuzo za Watendaji Wakuu Bora 100 wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni jana.

Tuzo za Watendaji Wakuu Bora 100 wa Mwaka zinalenga kuwaangazia viongozi wa kipekee kutoka mashirika ya kifaida na yasiyo ya kifaida, kwa kuwatia moyo washiriki kushirikisha hadithi zao za mafanikio hivyo kuleta hamasa kwa viongozi wengine.
Tuzo hizi, zinazoratibiwa na taasisi ya Eastern Star Consulting Group, zinalenga kutambua na kusherehekea mafanikio ya kibinafsi na ya mashirika yao kupitia viongozi hao wenye utendaji uliotukuka nchini Tanzania.