Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Alipotembelea Banda la SBL
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri alipotembelea banda la Serengeti Breweries Limited hapo jana kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. SBL amekua ni mdau mkubwa katika sekta ya uwekezaji nchini kwa kuwasaidia kuwainua kiuchumi wakulima wa mazao ya shayiri, mtama na mahindi; mazao ambayo yanatumika kama malighafi ya utengenezaji wa bia.