Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Tanga Atangaza Nafasi za Kazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
1.1 MTENDAJI WA MTAA DARAJA III – NAFASI 6
1.1.1 KAZI NA MAJUKUMU:
i. Mtendaji Mkuu wa Mtaa;
ii. Mratibu na msimamizi wa upangaji wa mipango shirikishi ya maendeleo ya Mtaa;
iii. Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa;
iv. Msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na sheria nyingine zinazotumika
katika Mtaa;
v. Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama;
vi. Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na
umaskini katika mtaa;
vii. Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za
walipa kodi wote;
viii. Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa na;
ix. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha IV/VI waliohitimu Astashahada (NTA Level 5) katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii (Sociology), Usimamizi wa Fedha (Finance Management), Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS C.
1.2 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5
1.2.1 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
vi. Kufanya usafi wa gari; na
vii. Kufanya kazi nyingine kadri utakavyoelekezwa na Msimamizi wako
1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya kidato cha nne(iv) au sita (form six), awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali,Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.
1.2.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS B
1.3.3 MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII DARALA LA II – NAFASI 1
1.3.3 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kusaidia na kupanga mipango na Miradi ya Maendeleo katika eneo lake.
ii. Kusaidia uwezeshaji na upatikanaji wa mafunzo kuhusu masuala ya
maendeleo katika eneo lake.
iii. Kusaidia kutoa elimu kuhusu kazi za kujitegemea katika eneo lake.
iv. Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
v. Kuandaa na kutoa taarifa za kazi za maendeleo ya Jamii kila mwezi kwa
uongozi wa kijiji na kwa msimamizi wake wa kazi.
vi. Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na vya kimaendeleo
vii. Kutambua na kuwezesha Kaya maskini kuinua uchumi wao kupitia fursa na
rasilimali zinazowazunguka.
viii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Waombaji wenye cheti cha mtihani wa kidato cha nne (IV) au sita (VI ) wenye Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
Maendeleo ya Jamii (Community Development), Sayansi ya Jamii (Sociology), masomo ya Maendeleo (Development Studies), Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project
Planning and Management), Jinsia na Maendeleo (Gender and Development), Rural Development au fani nyingine zinazofanana na Maendeleo ya Jamii.
1.3.3 NGAZI YA MSHAHARA TGS B –
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na
wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza
(DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina
ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iv. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa
zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V)
yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
vi Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa
kuzingatia sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
vii. Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo
ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezoyaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,
2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua
za kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 07 Agosti, 2024.
4
xiii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
–
Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji la Tanga,
S.L.P 178,
TANGA
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
xv.Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
Imetolewa na;
Dkt. Frederick Sagamiko
MKURUGENZI WA JIJI
HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA